Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 24 Machi, 2025 Ikulu ndogo ya Mkanyageni, Chake Chake, mkoa wa Kusini Pemba.
Mkutano huu ni wa pili kufanyika baada ya ule wa
kwanza uliofanyika tarehe 08 Februari, 2025 Ikulu, Jijini Dar es Salaam na
ulihudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali wafuatao:-
Rais William Ruto wa Kenya, Dkt. Emmerson Mnangagwa wa
Zimbabwe, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Yoweri Museveni wa
Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Lazarus Chakwera wa Malawi, Rais Andry
Rajoelina wa Madagascar, Rais Hakainde Hichilema wa Zambia, Dkt. Samia Suluhu
Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri Mkuu wa Somalia
pamoja na Mawaziri kutoka Sudani Kusini na Angola.
No comments:
Post a Comment