Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Sheikh Juma Makungu Juma (katikati)akiwa pamoja na Viongozi wengine wakiomba Dua katika Kaburi la Meja Jenerali Mstaafu Marehemu Abdalla Said Natepe aliezikwa Kijijini kwao Mwachealale Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Kaskazini Unguja.Ikiwa ni Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa Chama Cha Afro Shirazi pamoja na Siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.Dua ilioongozwa na Sheikh Sharif Abdurahman Muhidini kutoka Ofisi ya Mufti.
Na Rahma Khamis -Maelezo Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar Mhe Juma Makungu Juma amesema Serikali ya awamu ya nane itaendelea kuwaenzi na kuwakumbuka waasisi wa Mapinduzi ili kuthamini michango yao katika kupigania nchi.
Ameyasema hayo wakati alipotembelea na kumwombea dua Mwasisi wa Mapinduzi Meja Jenerali Mstaafu Marehemu Said Natepe huko Mwachealale Wilaya ya Magharibi ‘A’.
Amesema kuwa lengo kufanya dua ni kuwaenzi viongozi waliojitolea kwa hali na mali bila ya kuogopa na kujenga nchi kwa kuikomboa na kuweka amani na utulivu pamoja na kuleta maendeleo.
“Tunajifunza kuwa wazalendo kwani hawa ndio wazalendo walioendeleza nchi yetu”, alisema Naibu Waziri.
Aidha ameitahadharisha jamii kujitahidi kuishi kwa kufanya matendo mema na kuacha historia nzuri ili iwe kumbukumbu wakati wataondoka duniani sio kujiachia kama kwamba wataishi milele.
“Sisi tujiulize tukiondoka duniani tutakumbukwa kwa lipi hivyo ni wajibu wetu kufanya mazuri ili tukifa tukumbukwe kwa mazuri yetu.” alikumbusha Naibu Makungu.
Nae mtoto wa marehemu Ali Natepe ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana kwa hali na mali na kuiomba kuendeleza ushirikiano wao wa kuwakumbuka wazee waliotangua kwa kuwaombea dua na kutakia mema ili wapate kufanikiwa zaidi.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Sheikh Juma Makungu Juma akitoa hotuba katika hafla ya Dua ya kumuombea Meja Jenerali Mstaafu Marehemu Abdalla Said Natepe aliezikwa Kijijini kwao Mwachealale Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Kaskazini Unguja.Ikiwa ni Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa Chama Cha Afro Shirazi pamoja na Siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.
Baadhi ya Wageni Waalikwa na wanafamilia waliohudhuria katika Dua ya kumuombea Meja Jenerali Mstaafu Marehemu Abdalla Said Natepe aliezikwa Kijijini kwao Mwachealale Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Kaskazini Unguja.Ikiwa ni Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa Chama Cha Afro Shirazi pamoja na Siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.
Baadhi ya Wageni Waalikwa na wanafamilia waliohudhuria katika Dua ya kumuombea Meja Jenerali Mstaafu Marehemu Abdalla Said Natepe aliezikwa Kijijini kwao Mwachealale Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Kaskazini Unguja.Ikiwa ni Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa Chama Cha Afro Shirazi pamoja na Siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Sheikh Juma Makungu Juma (KULIA)akimkabidhi Kiongozi wa Familia ya Meja Jenerali Mstaafu Marehemu Abdalla Said Natepe Ali Natepe Bahasha Maalum ya Sadaka ya Serikali katika hafla ya kumuombea Dua Marehemu huyo iliofanyika Kijijini kwake Mwachealale Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Kaskazini Unguja.Ikiwa ni Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa Chama Cha Afro Shirazi pamoja na Siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.
PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR.02/04/2025
No comments:
Post a Comment