Habari za Punde

WAZIRI MHAGAMA AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA FALME YA ESWATINI

 AFYA2332.JPG

Waziri wa Afya na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jenista Mhagama leo Aprili 15, 2025 amewasilisha ujumbe maalum kwa Ufalme wa Eswatini ambao umepokelewa na Waziri Mkuu wa Falme hiyo Mhe. Russell Mmiso Dlamini Jijini Mbabane, Eswatini.

Waziri Mhagama ameushukuru Ufalme wa Eswatini kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuendeleza ushirikiano mzuri wa Kidiplomasia uliopo baina ya Mataifa hayo mawili.

Waziri Mhagama ameambatana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji anayewakilisha Tanzania pia katika  Falme ya Eswatini Bw. Ali Ubwa Mussa pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace, Magembe.

AFYA2322.jpg

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.