Habari za Punde

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Azungumza na Ujumbe wa Kamati ya Amani Zanzibar

Na.OMKR. Zanzibar.  

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba wazanzibar na wadau wengine wa uchaguzi wa Zanzibar wanaendelea kuwa na wasiwasi na mashaka yanayoweza kutokea kwenye  uchaguzi mkuu ujao kama yalivyotokea kwenye chaguzi nyengine.

Mhe. Othman ameyasema hayo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar alipokutana na kufanya mazungunzo na Kamati ya Amani inayoongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar  inayowashirikisha viongozi mbali mbali wa dini ya Kiislamu na wakrito.

Mhe. Othman amesema kwamba suala hilo linatokana na kuendelea kuwepo viashiria na vitendo vinavyokosesha haki baadhi ya wananchi jambo amnalo ndio chanzo kikubwa cha kuvurugika kwa Amani kabla na baada ya uchaguzi.

Amesema kwanzishwa kwa kamati hiyo ni jambo jema lakini kinachohitajika ni kuwepo nia thabiti katika na dhamira ya kweli ya kuyakabili mambo yote yanayoleta mkanganyiko wa Amani kwa watu wa Zanzibar katika miongo mitatu ya uchaguzi uliopita.

Amesema kwamba Nchi mbali za Afrika wamefanya iuchgazi licha ya kwamba vyama tawala na vilivyopigania uhuru na ukombozi wa nchi zao wameshindwa na kuwapongeza walioshinda na nchi zikaendelea kuwa na Amani pamoja na kuendelea kuongoza nchi kwa kutumia mfumo wa serikali za umoja wa kitaifa kwa zaidi ya vyama kumi.

 

Mhe. Othman amefahamisha kwamba tafauti ya wazanzibari inapadnikizwa  wa watu wanaodhani kwamba nchi hiyo sio ya wote bali inawahusu kundi ama watu Fulani wenye mnalaka ya kwamba lazima wawe wao kwenye madaraka hata kama wameshindwa.

Amesema kwamba kamati hiyo ya Amani kwa maoni yake bado haijafanikiwa kwa sababu chanzo kinacholeta migogoro ya Zanzibar ni kutokuwepo haki kwa watu kunyimwa haki zao ikiwemo suala la vitambulisho.

Amesema ili kustawisha Amani kabla na baada hya uchaguzi ni la zima kamati hiyo kujikita kwa kuyaeleza baya na wazi wazi kwa viuongozi wote amabo ndio chimbuko la kuvunjika kwa Amani ya Zanzibar kabla na baada ya uchaguzi.

Ameeleza kwamba hakuna ngombe anayeweza kuchinjwa kwa mkiani na kwamba kama hiyo inapaswa kwenda  na kuyaeleza kwa undani masuala ambayo jamii na viongozi wa siasa wanaamini na kufahamu kwamba ndio chimbuko la kukosekana haki ikiwemo mifumo ya tume ya uchaguzi sharia na viongozi waiso waaadilifu katika kusimamia uchaguzi wa Zanzibar.

Amesemisitiza kwamba Amani ya Zanzibar ni si sisasa bali ni uchumi kutokana na ukweli kwamba wawekezaji wengi duniniani hasa kwenye nchi ya visiwa kama Zanzibar  ambayo uchumi wake unategemea huduma Amani ni jambo la kwanza linalozingatiwa na wenye fedha duniani kote.

Amesema kewamba jukumu namba mnoja ni watu kuwa na fursa ya kufanya mambo yao kwa utulivu na kwamba inapokuwa hakuna Amani hata majina ya watu yanabadilishwa wengine wakaitwa wakimbizi.

Ameitaka kamati hiyo kuhakikisha kwamba wawafikia wadau mbali mbali  na kutumia maarifa yao na weledi alionao ili kusikia kutoka kwenye midomo yao kufahamu chanzo halisi cha mizozo na kuvunjika kwa Amani ya Zanzibar ili kuweza kufanikiwa dhamira na lengo la kuundwa kamati hiyo.

Mapema Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab akiyeongoza ujumbe huo amesema kwamba kamati hyo iliyoundwa na viongozi wa dini katika pande zote kwa dhamira ya kujenga Amani Zanzibar kabla na baada ya uchaguzi.

Kwa Upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wokfu na Mali ya Amani Zanzibar sheikh Abdalla Talib  amesema kwamba kamati hiyo imeundwa kutokana na kuwepo histori ya kuvunjika kwa Amani kwa vipindi vyote vya uchaguzi.

Mwisho.

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari Leo Ijumaa tarehe 02 Mayi 2025.

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.