Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amemuapisha Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Kombo Hassan Juma kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar, hafla hiyo ya uapisho iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 15-5-2025, na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
KOMBO Haasan Juma akiapa kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 15-5-2025
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisaini hati ya kiapo ya Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar, Kombo Hassan Juma, baada ya kumuapisha katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 15-5-2025 na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.