Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab akizungumza na Wazee na Walezi wa Watoto wakati wa hafla ya ufunguzi wa Madrasa ya Jumuiya ya Zawiyatul-Qadiriya Michamvi Pingwe Mkoa wa Kusini Unguja.

Ametoa wito huo wakati alipokuwa akifunguwa Madrsa ya Jumuiya ya Zawiyatul-Qadiriya Tanzania kwa upande wa Wanawake, iliopo Michamvi Pingwe Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema iwapo Wazazi na Walezi hawatoshirikiana na Waalimu ipasavyo, Watoto wao hawatoweza kupata elimu kama inavyotakiwa.
Aidha amesema kwa wakati huu, kumekuwa na changamoto nyingi zinazowakabili Wanafunzi hivyo amewataka Wanafunzi kuwacha usiri na kuelezeza changamoto, zinazoashiria kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji.
Hata hivyo Katibu Fatma, ameahidi kushirikiana na kuwa bega kwa bega na Uongozi wa Madrsa hiyo ili iweze kuendelea na kutoa elimu kama ilivyokusudiwa.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Madrasa hiyo Ust. Hafidh Ali Khamis amewaomba Wazazi kusimamia maendeleo ya Watoto kwani baadhi ya Wanafunzi wanakimbia masomo ya Madrsa kwa ajili ya kuenda Pwani.
Hata hivyo amewaomba Wafadhili na Watu wenye uweze kujitokeza kuiunga mkono Madrasa hiyo ili iweze kufikia malengo iliojipangia ya kutoa elimu bora kwa Wanafunzi wake.
Akisoma Risala katika Ufunguzi wa Madrasa ya Jumuiya zawiyatul Qadiriya Tanzania Michamvi Pingwe amesema Madrasa hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa Mota ya kuvutia Maji jambo ambalo linawapa usumbufu wa kuchota Maji kwa Ndoo.
Madrasa ya Jumuiya Zawiyatul- Qadiriya Tanzania iliopo Michamvi Pingwe Wilaya ya Kusini, imeanzishwa mwaka 2020, ikiwa na Wanafunzi wa 4 ambapo kwa sasa ina jumla ya Wanafunzi 100, chini ya Uongozi wa Ustadh. Hafidh Ali Khamis.
Imetolewa na Kitengo cha Habari,
WHVUM.
No comments:
Post a Comment