Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Akimuwakilisha Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Kuzungumza na Waratibu wa Uchuguzi Ukumbi wa ibirinzi Chakechake Pemba

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla akizungumza katika Mkutano wa waratibu wa shughuli za Uchaguzi wa Mikoa miwili ya Pemba uliofanyika katika Viwanja vya Tibirizi Wilaya ya Chake Chake Pemba.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amewataka wajumbe wa Kamati za Uratibu za uchaguzi katika shehia zote za Pemba kuhakikisha wanasimamia vyema dhamana waliyopewa ya kusimamiaushindi wa Chama cha mapinduzi ifikapo Oktoba 29.

Ameyasema hayo kwa niaba ya Makamun Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Mkutano wa waratibu wa shughuli za Uchaguzi katika Mikoa miwili ya Pemba uliofanyika katika Viwanja vya Tibirinzi Chake Chake Pemba.

Amewataka waratibu hao kuwa na utayari wa  kuutimia vyema utaalamu waliopatiwa katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuhakisha wanasimamia ushindi wa chama cha mapinduzi.

Ndugu Hemed amewataka kudumisha nidhamu wanapokuwa katika majukumu yao kwa kuwa wanyenyekevu na kutumia lugha za kistaarabu ili kuwapa uhuru wapiga kura kupiga kura kwa Imani na Utulivu mkubwa.

Ndugu Hemed anefahamisha kuwa CCM itaandaa utaratibu mzuribu mzuri kuhakikisha wazee, wagonjwa na wasiojiweza wanafika salama katika vituo vya kupigia kura wakiwa na uaangalizi na usimamizi wa kutosha katika kutekeleza haki yao hio ya kikatiba.

Aidha, amesema watahakikisha katika maeneo yote huduma muhimu na stahiki zinapatikana na kuziondosha chamgamoto zote zinazoweza kuathiri  utaratibu mzima wa zoezi la uchaguzi.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Afisi Kuu za CCM Kisiwandui Dkt. Khalid Salum Muhammed amesema lengo la mkutano huo ni kuwakumbusha waratibu wa uchaguzi majukumu yao ikiwemo kuendelea kuzisaka kura za wagombea wote wa CCM pamoja na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika zoezi la kukipigia kura chama cha Mapinduzi.

Dkt. Khalid amewataka waratibu hao kukataa kurubuniwa na kushawishiwa kwa namna yoyote ile itakayopelekea kukisaliti chama na badala yake waendelee kukisimamia mafunzo waliyopatiwa ili kukiletea ushidi Chama cha Mapinduzi.

Amewaasa kuacha ugonvi, makundi na mifarakamo baina yao na kuwataka kudumisha umoja na mshikamano katika majukumu yao ya kukisimamia na kukipigania chama kiweze kushinda kwa kishindo.

Katibu wa Kamati Maalum (NEC) Idara ya Oganaizesheni ndugu Omar Ibrahim Kilupi amesema Ulinzi na Usalama utainarishwa maradufu katika kipindi chote cha uchaguzi na kuwatoa hofu wana CCM na wananchi kwa ujumla kuwa hakuna uchafuzi wowote wa amani   utakaotokea na uchaguzi utafanyika kwa amani na usalama mkubwa.

Kilupi amewaomba wanaCCM na wananchi wote kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kuwahimiza ndugu na jamaa zao kushiriki katika zoezi la kupiga kura  na kukichagua Chama cha Mapinduzi ili kiendelee kushikilia dola na kuzidi kuiletea maendeleo nchi yetu.

Amewataka wagombea wote wa CCM kuendelea kufanya kazi zaidi katika kipindi kilichobakia ambacho ni kipindi muhimu cha kuwafikia wananchi katika maeneo yao pasipo kujali itikadi zao na kuwaomba kukipigia kura chama cha Mapinduzi ifikapo Oktoba 29.

KILUPI amewaomba wanaCCM na wananchi wote kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kuwahimiza ndugu na jamaa zao kushiriki katika zoezi la kupiga kura  na kukichagua Chama cha Mapinduzi ili kiendelee kushikilia dola na kuzidi kuiletea maendeleo nchi yetu.

Amewataka wagombea wote wa CCM kuendelea kufanya kazi zaidi katika kipindi kilichobakia ambacho ni kipindi muhimu cha kuwafikia wananchi katika maeneo yao pasipo kujali itikadi zao na kuwaomba kukipigia kura chama cha Mapinduzi ifikapo Oktoba 29.

Nae Mratibu wa shughuli za Uchaguzi Pemba Bi Mauwa Abeid Daftari amesema zoezi la kukiombea kura Chama cha Mapinduzi linaendelea vizuri kwa Mikoa Miwili ya Pemba ambapo kila walipopita muitikio wa wananchi wanaoahidi kuipigia kura CCM ni mzuri na hawana hofu na ushindi wa CCM  Kisiwani Pemba.

Bi Mauwa amesema wamejipanga kimikakati  kuhakikisha majimbo yote ya Pemba yanabakia katika Mikono ya CCM na wameahidi kuwa hakuna jimbo hata moja litakalochuliwa na chama cha upinzani.

Imetolewa na kitengp cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe 22 / 10 /2025.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.