6/recent/ticker-posts

TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR YAKABIDHIWA BENDERA KUWAKILISHA CECAFA.

 Waziri Habari Michezo Utamaduni na Utalii Abdillah Jihad Hassan, akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar kabla ya kuwakabidhi Bendera kuiwakilisha Zanzibar katika Mashindano ya Afrika Mashariki Mjini Dar-es-Salaam, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni.  
 Mfadhili Mkuu wa Timu ya Taifa ya  Zanzibar wa Kampuni ya Future Centery Bi Helena, akitowa nasaha zake wakati wa kuiaga Timu ya Taifa ya Zanzibar katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Kikwajuni.
 Waziri wa Habari,Michezo Utamaduni na Utalii Abdillah Hassan Jihad, akimkabidhi Bendere Nahodha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Agrey Morris, ili kuiwakilisha Zanzibar katika michuano ya Kombe la CECAFA mjini Dar-es-Salaam.
 WAFADHILI wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Michezo, Abdillah Hassan,(kushoto) Ibrahim Attas, (ZANTEL) Collins Chengoren, (United Petroleum zanzibar) Mohamed Mussa (ZANTEL) na Amour Juma (Benki ya Watu wa Zanzibar).
 Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakiwa makini kumsikiliza Waziri wa Michezo Abdillah Jihad akitowa nasaha zake kwa Wachezaji  hao jana
 Waziri wa Michezo Abdillah Jihad akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakati wa hafla ya kuwakabidhi bendera ya kuiwakilisha Zanzibar.
 Makamu Mwenyekiti wa ZFA Alhaj Ameir, akitowa shukrani kwa niaba ya Chama cha Mpira cha Zanzibar ZFA, baada ya kukabidhiwa bendera ya kuiwakilisha Zanzibar, na kuahidi kurudi na ushindi wa Kishindo na bendera kupepea. 
 Makocha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Hemed Moroco na Abdulfatah Abass, wakimsikiliza Waziri wa Michezo akitowa nasaha zake kwa wachezaj, ukumbi wa Wizara ya Habari Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni.   
MENEJA Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Amour Juma, akimkabidhi cheki ya Shillingi Milioni Mbili kwa Mfadhili Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar Bi. Helena, wakati wa makabidhiano ya bendera.    
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya United Petroleum Collins Chengorey, akitowa shukrani kwa niaba ya Wafadhili wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, wakati wa kuiaga timu hiyo na kuikabidhi Bendera. 
 Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Utalii Abdillah Jihad, akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Taifa ya Zanzibar.
 KOCHA wa timu ya Taifa ya Zanzibar Abdulfatah Abass, akibadilishana mawazo na Waziri wa Michezo Abdillah Jihad, baada ya kuiaga timu hiyo.  
 Wafadhili wa timu ya Taifa ya Zanzibar wakibadilishana mawazio nje ya ukumbi baada ya kumalizika makabidhiano ya bendera na kuiaga Timu ya Taifa ya Zanzibar.   

Post a Comment

0 Comments