6/recent/ticker-posts

Dk Bilal afungua kituo cha Polisi Kiboje

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Mohamed Gharib Bilal akikabidhi cheti cha shukrani kwa Saleh Mohamed Said
kutokana na msaada wake wa kufadhili ujenzi wa kituo cha polisi cha Kiboje mkoa wa kusini Unguja kwenye ufunguzi uliofanyika juzi.
Kampuni ya Migozi Supermarket ya mjini Zanzibar inayomilikiwa na Saleh imechangia ujenzi huo uliogharimu sh.milioni 50.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaliminana na maofisa wa Usalama wa Wilaya ya Kati, wakati alipowasili eneo hilo kwa ajili ya kufungua rasmi Kituo cha Polisi cha Kiboje, kilichpo Mkoa wa Kusini Unguja leo Desemba 26, 2012
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala na Kamishina wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa, wakifunua kwa pamoja kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho ulioanza Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, wakati akitembelea kukagua jengo la Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kufungua rasmi jengo hilo lililoanza kujengwa Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja

Picha na OMR

Post a Comment

0 Comments