6/recent/ticker-posts

Mradi wa Uchimbaji wa Visima Makunduchi Wapambamoto chini ya Mwakilishi Wao Mhe. Haroun Ali Suleiman.


Mwakilishi wa Jimbola Makunduchi Mhe. Haroun Ali Suleiman, akimsikiliza Sheha wa Shehia ya Mzuri Nd.Mwita Masemo, wakati mafundi wa Kampuni ya Uchimbaji wa Visima ya Chimba wakifunga mitambo ya uchimbaji wa kisima hicho leo katika shehia ya Mzuri.

Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wa Uzinduzi wa uchimbaji wa kisima cha Maji katika shehia ya Mzuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.
Wawawa wananchi wa Mzuri Makunduchi kwa Mradi wa uchimbaji wa Visima vya Maji Safi na Salama kwa Watumizi 
Wananchi wa Mzuri Makunduchi wakishuhudia uchimbaji wa Kisima hicho katika shehia yao leo wakati wa kuaza kwa mradi huo na kupata furaha na faraja ya kupata mradi huo katika jimbo lao kutokana na jitihada za Mwakilishi wao kulipatia maendeleo jimbo lake katika mahitaji ya Jamii inawafikia kwa wakati muafaka.
Wananchi wa Jimbo la Makunduchi wakifuatilia uchimbaji wa Kisima chao kipya katika shehia ya Mzuri, uchimbaji wa kisima hicho umeaza leo na kujitokeza wakazii wa shehia hiyo kushuhudia mradi huo wakiwa na Mwakilishi wao Mhe. Haroun Ali Suleiman. Mradi huo wa uchimbaji wa visima vitatu katika jimbo hilo utapunguza na kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wingi kusaidia visima vilioko katika jimbo.
Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza na Wananchi wake wakati wa Uchimbaji wa Kisima kjatika Kijiji cha Mzuri Makunduchi, mradi wa uchimbaji wa Visima hivyo Vitatu unaozihusisha vijiji vya Mzuri Mtende na Uwandani, kuongeza upatikanaji wa Maji kwa wananchi wa jimbo hilo, kusaidia visima vingine Vinane vilivyochimbwa na Mwakilishi huyo kushirikiana na Wananchi wa jimbo lake. Visima hivin vitatu ni mradi Mkubwa wa visima 50 vilioko katika Mradi wa Nchi ya Ras Al Khaimah kwa ajili ya huduma ya kuchimba Visima katika Maeneo ya Unguja  na Pemba.
Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Shehia ya Mzuri Issa Ame, Amesema mradi huu utattulikuwa tukiusubiri kwa hamu kubwa ili kupata ongezeko la maji kwa Shehia yetu, ili kusaidia upatikanaji wa maji kwa wingi katika maeneo yetu na kuweza kumwagilia mazao yetu katika mashamba ikizingatiwa sehemu kubwa ya kilimo chetu tunategemea maji.

Post a Comment

1 Comments

  1. hapa inaonyesha kama vile wanachimba kisima , hivh kweli ndio mafanikio haya ya mapinduzi ya miaka hamsini ? mpaka leo maji yametushinda kuyasambaza katika eneo dogo ambalo hata halifikii mkoa mmoja wa bara? na huku tunajenga mnara wa kukumbuka miaka 50 kwa kutumia mabilioni ya fedha za wananchi jee ni haki? au ni mnara wa kutukumbusha tulivyofeli katika sera zetu?

    ReplyDelete