Na Mwajuma Juma
MAAFANDE wa timu ya Polisi wameilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 timu ya Miembeni ‘Kwala’ katika mchezo wa ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt uliochezwa Mao Tse Tung mjini hapa.
Miamba hiyo ambayo ilishuka uwanjani hapo majira ya saa 10:3 0 za jioni ilionekana kushambuliana kwa zamu hali iliyoleta ushindani mkali kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo huo.
Miembeni kwa matokeo hayo imefikisha 15 na kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ambayo inaongozwa na Mtende Rangers kwa kuwa na pointi 16.
Katika mchezo huo timu hizo ambazo zinaushindani wa jadi ziliuanza mchezo kwa kasi na kupelekea mashabiki waliohudhuria mchezo huo kuvutiwa nao.
Miembeni ilitangulia kupata bao la kuongoza katika dakika ya 13 lililofungwa na mchezaji wake Omar Tamimu na kusawazishiwa katika dakika ya 89 kupitia kwa mchezaji Mohammed Hassan.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo uwanjani hapo kwa mchezo kati ya ndugu wawili Mafunzo na Zimamoto

0 Comments