Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na Naibu Kadhi Mkuu Sheikh Hassan Othman Ngwali (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Pemba Juma Khamis wakimsalia Mtume katika hafla ya Maulid yaliyofanyika Tumbatu Jongowe. (Picha na Salmin Said, OMKR).
Na Khamis Haji, OMKR
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amewahimiza wananchi wa Zanzibar kuungana katika kulinda na kuhifadhi utamaduni, mila na silka za Wazanzibar, ili kuepusha tabia ya kuipotosha kwa makusudi inayofanywa na baadhi ya watu.
Maalim Seif ameyasema hay oleo, wakati alipokuwa akihutubia katika hafla ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), yaliyoandaliwa na Madrasat Nur Islamiya huko katika kijiji cha Tumbatu Jongowe, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja.
Amesema utamaduni na mila za Wazanzibari ni za kipekee na vuimerithiwa kwa miaka mingi, lakini baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kuvipotosha kwa malengo maalum, jambo ambalo linapaswa kupigwa vita na wananchi kulikataa.
Amesema historia ya Zanzibar ina mafungamano makubwa na Dini ya Kiislamu kwa zaidi ya miaka 1000, hali ambayo inathibitishwa na kuwepo maeneo mengi ya kihistoria, ikiwemo msikiti wa Kizimkazi, magofu ya majengo ya asili huko Makutano katika kisiwa cha Tumbatu, pamoja na athari za iliyopo katika eneo la Kihistoria la Mkuu, kisiwani Pemba.
Aidha, Makamu wa Kwanza wa Rais amesema malengo hayo yataweza kufikiwa iwapo Walimu, Masheikh na Wazee watakuwa na tabia ya kuwafunza watoto wao historian a utamaduni wa nchi yao.
Makamu wa Kwanza wa Rais pia ametumia hafla hiyo kuhimiza umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari wote hasa wakati huu wa kutafuta Katiba mpya ya Tanzania, ili kuweza kulinda maslahi na musatakabala mwema wa Zanzibar.
“Tukishikamana tutakuwa wamoja, tutaweza kutetea na kulinda maslahi ya nchi na watu wake, tukigawana na kuweka mbele maslahi binafsi, badala ya kuweka mbele maslahi ya Taifa tutashindwa kuitumia vyema fursa hii”, alisema Maalim Seif.
Katika risala yao wana Madrasa hao wa Nur Islamiya waliwapongeza wananchi na viongozi mbali mbali, kutokana na michango yao iliyowezesha Madrasa hiyo kujengwa katika kipindi kifupi.
Katika risala hiyo iliyosmwa na Maalim Juma Makame, waliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali, pamoja na wananchi wa kijiji hicho katika kuwajenga watoto katika maadili mema, ili wawe wananchi wema wanaoweza kutegewa na Taifa.
Nae, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali akihutubia katika hafla hiyo, amewahimiza waumini wa Kiislamu kuzidisha bidii katika kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W), na kushikamana na mafundisho yake kivitendo.
Maulid hayo ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) hufanyika kila mwaka ifikapo mwezi 12 Mfunguo tatu.

3 Comments
nafikiri ndugu kadhi kama ni mwadilifu wa kweli kawaambie viongozi wa serikali wanaotutawala kwanza wao washikamane na mafunzo ya Mtume SAW kivitendo , waache kujunufaisha na nafasi walizopewa , waambie Mtume SAW hakuwa na jeshi la kumlinda, wala hakukaa katika ikulu au jumba la kifahari , wala hakuchukua senti ya shaba katika hazina ya himaya yake akitafuta riziki yake kwa kufanya kazi , wala hakuwa na watumishi wala walinzi wa kumlinda , wala hakuchukuwa posho kwa kukaa vikao , wala hakutumia fedha/mali ya umma kwa faida yake au ya familia yake , wala hakuitwa mheshimiwa , watu waliochini yake hawakuwa wakisimama kama akiwa anapita au kuwatokezea. Jee ndugu kadhi unaweza kuwaambia haya hao waliokuajiri kama mwadilifu na unamtegemea na kumwamini Mungu ? haya machache wakiweza kuyafata tutapiga hatua kubwa na watu wa chini akina sisi walalahoi tutaiga , mfano wowote uanzie juu kushuka chini. Mawaidha haya kawape viongozi wote wa serikali na idara na mawizara huko ndiko kwenye utovu wa nidhamu sio kuwahutubia walalahoi sisi japo vipi riziki zetu ni za halali.
ReplyDeleteNdugu mtume Saw alikuwa ana ongoza dini sio serekali, sas makamo wa kwnza kenda pale kama ualikwa na kuwa yeye ni muumini wa kislam, lakini dola anayo iongoza si yakii slam na wala sisi wenyewe hatutaki iongozwe hivyo, yeye katumia wajibu wake kama muumin, kujilisha wasiache mila na silka zadini yao, hata kama angealikwa kanisani ilikuwa ni wajibu kuwambi wakiristo wafate maadili aliyo wafundish yesu, sas tusi iyandeme, kwadini, tuindame kwa wizi unao fanya ndani gnu, hivi sas unatisha hakuna wakumlaumu mwenziwe wote wivi ccm na cuf, na utawala wa kidini hauji milele, mpa ka uanze maka znz iwe ya pili kimeme wanaota kuwamuadilifu ni yule anaye fata vitendo vya mtume kwa hajui waha ccm na cuf wana swali na kufunga mbona wanagombana kwa kuiba mali za walipakodo matumbo hayo kama mapipa
ReplyDeletendugu kitine Mtume SAW alikuwa na utawala kama hujui kasome , nafikiri umechanganya habari au hukuelewa niliyoandika , sijasema ujue utawala wa kidini hapa znz angalia vizuri nimeandika nini , na mambo gani ya kuigwa hapo juu na viongozi wezi wa serikali yetu si yakidini bali ya binadamu aliyekamilika na mzalendo mwenye uchungu na raia wake kama alivyokuwa Mtume SAW
ReplyDeleteKalagha baho