6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL AWEKA JIWE KA MSINGI LA UJENZI WA NYUMBA 851 ZA WATUMISHI WA UMMA ENEO LA BUNJU 'B' WILAYA YA KINONDONO MKOA WA DAR.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba 851 za Watumishi wa Umma zinazojengwa katika eneo la Bunju B, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, wakati wa sherehe hiyo liyofanyika leo. Kutoka (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Miundombinu, Peter Serukamba, Waziri wa Ujnezi, Dkt. John Pombe Magufuli na (kushoto) kwa Makamu ni Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga na Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Bunju B, wakati alipofika kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba 851 za Watumishi wa Umma zinazojengwa katika eneo hilo, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, wakati wa sherehe hizo
 Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akizungumza machache na wananchi wa Bunju B, kabla ya kumkaribusha Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, kuwahutubia Wanancnhi hao, wakati alipofika kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba 851 za Watumishi wa Umma zinazojengwa katika eneo hilo, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga, wakati akikagua ramani za ujenzi wa Makazi ya Nyumba 851  za Watumishi wa Umma zinazojengwa katika eneo la Bunju B, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, wakati wa sherehe hiyo liyofanyika leo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi na TBA.12:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Vijana wa Kikundi cha Uhamasishaji, waliokuwepo katika sherehe hiyo, mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba 851 za Watumishi wa Umma zinazojengwa katika eneo hilo, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, wakati wa sherehe hiyo liyofanyika leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi wa Bunju B, wakati akiondoka eneo hilo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba 851 za Watumishi wa Umma zinazojengwa katika eneo hilo, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, wakati wa sherehe hiyo liyofanyika leo. Picha na OMR

Post a Comment

0 Comments