6/recent/ticker-posts

Msaada wako unahitajika kusaidia mayatima, Mombasa , Kenya


                     

Assalam alaykum warahmatullaahi wa Barakatuh
 
Ndugu Waislamu! Kama mtakavyoona kwenye picha hapo juu, hiyo ni nyumba yenye vyumba zaidi ya vine na baraza (sebleni) kubwa inayokodishwa. Kuna mama ambaye anaishi Mombasa Kenya amejitolea kuwalea watoto mayatima. Na mpaka sasa wamefikia idadi isiyopungua chini ya watoto 15 na bado mpaka sasa wazidi kuongezeka. Wanaishi nyumbani kwake ambapo nyumba yenyewe si kubwa, jambo ambalo linapelekea kuwepo kwa msongamano na vurugu ya hali ya juu. Pamoja na yote hayo, mama huyu amekuwa ni mwenye subra mpaka hivi leo, Allaah Amlipe kwa hilo.
 
Alhamdulillaah jirani kwake anapoishi kumepatikana nyumba ya kukodi. Nyumba yenyewe mmiliki ahitajia pesa 23.000 Kenya Shilling kwa kila mwezi. Sasa twawaomba ndugu zangu, tumsaidie mama huyu kila mmoja atoe kwa kiasi atakachokiweza ili tuhakikishe kila mwezi – kwa uchache – basi kupatikane angalau 23.000 Kenya Shilling kodi ya nyumba.
 
Lengo khaswa la kuwachukua watoto hawa mayatima, ni baada ya kuona mahali anapoishi ni mahali ambapo kwanza wakaazi wake wengi ni manaswara, hakuna msikiti wa sunnah karibu, kinyume chake Bid´ah na ukhurafi ndio vimetapakaa na kueneza. Ndio tukawa tumeonelea kuchukua watoto wadogo na tukaweka kipaumbele kwanza mayatima na wale ambao hali zao ni duni kabisa.
 
Mpaka hivi sasa, watoto hawa tayari wamekwishawekewa mwalimu wa kuwafunza kila siku: mafunzo yaliyojengeka juu ya ufahamu wa Salaf-us-Swaalih (wema waliotangulia). Na mimi nilikuwa katika watu ambao nilishuhudia hili na nilitoka kule harakati tumekwishazianza na tumepiga hatua kiasi fulani. Kwa hivyo, isije kueleka na baadhi ya watu kwamba jambo hili lina maslahi ndani yake au ni biashara inafanywa. Hasaa wakallaa.
 
Kama tunavyojua mahitajio ya watoto ni mengi. Na mimi nimepata nguvu na moyo wa kuwaandikia baada ya kuona hatua tumekwishapiga na juhudi ambayo tumekwishafanya: watoto wote hawa wanakula nyumbani kwake asubuhi na jioni, wanalala kwake (kwa kuwa nyumba hiyo muionayo hatujakuwa na uwezo wa kuikodi), kishawanunulia magodoro na uniform za madrasa na mengi anawafanyia na bado anaendelea kuwafanyia. Kwa hivyo kubwa analohitajia na kutoka kwa ndugu zake Waislamu na ambalo ni muhimu kuliko yote ni jinsi ya kuilipa nyumba hii ambayo twatarajia siku za mbele kuifanya madrasah ya watoto na watoto wahamie humo.


Na kuna mama ndugu ambao hivi punde tu wamekwishajitolea: pesa walizokuwa wametuma tumenunua magodoro, shuka za kujifunika na mito ya kulalia. Na yote hayo mtayaona hapo juu kwenye picha. Allaah Awalipe hawa waliojitolea popote walipo na Ajaalie ´amali hii iwe ni Swadaqa yenye kuendelea baada ya kufa kwao. Na wale ambao Hawakujaliwa lakini walikuwa na azma na nia ya kuchangia na kuendeleza jambo hili la kheri mbele, Allaah Awalipe kwa nia yao.

  •       Upande wa kina mama, yule ambaye anataka kuchangia, kuuliza swali na mengineyo, basi awasiliane na Fatmah Khalifah kupitia email yake: fkhalifa99@yahoo.com na namba yake ya simu ni: 00254723359681
  •           Kwa mwanaume yeyote mwenye swali anaweza kuwasiliana na mimi kupitia email yangu hii: khatwiyb@gmail.com



Wa swallaAllaahu ´alaa Muhammad, wa ´alaa Aalihi wa Aswhaabihi wa sallam. 

Post a Comment

0 Comments