Na Mwandishi wetu, Dodoma.
WAJUMBE wa Bunge la Katiba jana
walishindwa kujadili kanuni zitakazoongoza mkutano wa bunge hilo, baada ya
baadhi ya wajumbe kukosa nyaraka.
Wajumbe hao walikutana jana katika
mkutano wa kawaida wa kazi, lakini wakati nyaraka hizo zikigawiwa ilibainika
kuwa baadhi ya wajumbe wamekosa.
Hali hiyo ilimlazimu Mwenyekiti wa muda
wa bunge hilo, Pandu Ameir Kificho, kutangaza kuahirisha mjadala huo hadi
Jumatatu.
Wajumbe walikuwa wakutane jana na leo
kujadili kanuni hizo kabla ya kuzipitisha katika mkutano wa Jumatatu.
Kutokana na hali hiyo shughuli za
kupitisha kanuni ambazo zilipangwa
kufanyika Jumatatu sasa zitasogezwa mbele hali ambayo pia itachelewesha
uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo .
Spika wa zamani wa Bunge, Samuel Sitta,
anapewa nafasi kubwa ya kushinda nafasi hiyo, hata hivyo alisema hatachukua
fomu hadi atakapoziona kanuni zitakazomuongoza kuongoza bunge hilo .
Wakati huo huo, habari kutoka Dodoma
zinasema kuna mipango ya chini kwa chini inaandaliwa na wajumbe kujiongezea
posho, ingawa baadhi yao
wanapinga.
Wanaotaka kujiongeza posho wanadai
kiwango cha shilingi 300,000 kwa siku hakitoshi huku wanaopinga wakisema
zinatosha na nyengine kubaki.
Katika hatua nyengine wakati zoezi la
usajili wa wajumbe likiendelea ilibainika wajumbe wawili walijitokeza wakitumia
majina ya aina moja.
0 Comments