Na Fatuma Kitima, DSM
CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA),
kimesema ripoti ya utafiti wa ukatili wa
udhalilishaji wa kijinsia inaonesha Zanzibar
inaongoza kwa matukio ya ukatili wa kijinsi.
Utafiti huo umeonesha idadi ya wasichana wanaoolewa wakiwa na umri mdogo wa kati ya miaka 15 hadi 19 nchini ni asilimia 2.8.
Akizungumza na wanahabari Dar es Salaam
jana, Mjumbe wa Bodi ya TAMWA, Gladness Munuo, alisema mafaniko ya utafiti huo Zanzibar yametokana na wahusika kuwa wawazi katika kutoa taarifa zinazowahusu tofauti na Tanzania Bara
ambako kumekuwa na urasimu.
"Lengo la utafiti huu lilikuwa ni
kuangalia kiwango cha matukio ya ukatili
wa kijinsia katika wilaya 14 za Tanzania
Bara na sita za Zanzibar,” alisema.
"Utafiti ulijikita katika maeneo ya
ubakaji, ukeketaji, vipigo, kutelekezwa wanawake na watoto, mauaji ya vikongwe, ndoa na mimba za utotoni,"alisema.
Alibainisha kuwa utafiti huo ulifanywa na
wanahabari kwa muda wa siku 10 na kwamba umethibitisha bila Tanzania bado ina
kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia.
Alisema matukio
yaliyobainika wakati wa utafiti ni
pamoja na ndoa za utotoni, kuozwa kabla hawajajitambua, wanawake kupigwa na kutukanwa, wanaume kutekeleza familia, ndoa
za mitala, vipigo na mauaji

1 Comments
hizi data hazina ukweli ndugu yangu , usipotoshe jamii bure , kila siku wanawake wangapi tanganyika , huuawa na waume zao , huvunjwa au kuathiriwa viungo vya mwili , kukeketwa , kupigwa mpaka kuumizwa , jee umeingiza hizi kwenye takwimu zako? nyinyi huwa mnawaandama waisilamu kwa kila njia bila ukweli msitake kutupotosha hapa , ndugu wananchi wa znz amkeni hizi ni propaganda za chini chini tushazijuwa kutuandama kwa dini yetu maanake mtakuja kusema dini yetu ndio inachangia wakati sio kweli , nendeni kwenu bara huko na chama chenu feki
ReplyDelete