Na Mwandishi Wete.
Zaidi ya milioni 80 zanatarajiwa kutumika kwa mwaka wa Fedha
2014/2015 kununulia vigari vya Watoto wenye Ulemavu wa Viungo Zanzibar ili
viweze kuwasaidia hasawanapokwenda skuli.
Waziri wa Nchi Ofisi yacMakamu wa Kwanzawa Rais wa Zanzibar
Mhe, Fatma Ferej,aliyasema hayo jana katika ukumbi wa baraza lawawakilishi
chukwani,wakati akijibu suala la
nyongeza la Mwakilishi waJimbola Muyuni Mhe, Jaku Hashim Ayoub,
alipotaka kujuwa Walemavu wa viungo wamekuwa wakipata wakati mgumu sana hasa
kwaWatoto walemavu wanaosoma skuli kukosa usafiri wa kufikia skuli.
Alisema katika bajeti ya mwaka 2012/2013 Serekali ilitenga
jumla ya shilingi milioni 13 huku bajeti ya mwaka 2013/2014 ilitenga shilingi
milioni 200 na kununua vigari kwa ajili yawatu wenye ulemavu Zanzibar .
Aidha alisema hivi sasa Wizara yake imekuwa ikipita nyumba
hadi nyumba ili kuweza kuwapatia watoto hao huduma hiyo sambamba na kuwataka
jamii kuacha tabia ya kuwafisha watoto wenye ulemavu na badala yake kuwatoa nje
ili waweze kusaidiwa.
Akijibu suala la nyongeza lililoulizwa na Mwakilishi wacViti
Maalum Mhe.Raya Suleiman Hamad, alipotaka kujua ni kwa nini watoto wenye
ulemavu wamekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuuziwa vigari vya
kutembelea.
Waziri Ferej alisema Serekali haiuzi baskeli wala haitouza
bali hutoa bure kwa watoto hao
Nae Mwakilishi wa Tumbe Mhe Rufai Said Rufai, alitaka kujua
jambo gani linasababishwa na ulemavu wa viongo wakati wakati akiulizasaulila
nyongeza.
Waziri Ferej alisema kwa sasa Serekali haijafanya utafiti
juu ya watu wenye ulemavu ila inasemekana mtu huzaliwa nao au hupata ajali.
Akitoa takwimwi za watu wenye ulemavu,Waziri Fatma Ferej,
alisema jumla ya watu 9,502 wenye ulemavu wa aina mbalimbali kwa Unguja na
Pemba ambapo kati ya hao wapo watu wenye ulemavu wa Ngozi,Uoni,Uziwi na
Viongo.
0 Comments