6/recent/ticker-posts

Fainali Kombe la Muungano Jimbo la Kiembesamaki Zenj.

Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki Mahmoud Thabit Kombo akifafanua mpangilio wa zawadi zitakavyotolewa kwa washindi na washiriki wa Kombe la Muungano lililoandaliwa ndani ya Jimbo hilo.Kushoto yake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mahindano hayo Juma Kocha.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Kikombe pamoja na baadhi ya zawadi Kepteni wa Timu ya Soka ya Chukwani United Mohd Golo baada ya Timu yake kushinda mchezo wa Fainal kwa goli 2-0 dhidi ya New Generation.
Wachezaji wa timu ya soka ya Chukwani United wakishangiria ushindi wao dhidi ya Timu ya New Generation iliyoupata wa Goli 2-0 kwenye mchezo wa fainali wa mashindano ya Kombe la Muungano lililoandaliwa ndani ya Jimbo la Kiembe Samaki.
Timu za Chukwani United iliyovalia jezi rangi nyekundu na New Generation zikimenyana ndani ya dimba la Kiembe samaki katika mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano ambapo chukwani United ilitawadhwa kuwa bingwa wa kombe hilo kwa kuichakaza New Generation goli 2-0 (Picha na Hassan Issa OMPR)

Post a Comment

0 Comments