Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar amesema kuwav hakuna
sababu yoyote nzito ya kutunga sheria juu ya wananchi wanaovyunja sheria katika
mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali
Mbarouk, alisema hayo jana barazani kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Abubakar Khamis Bakar, katika kikao hicho cha baraza la Wawakilishi wakati
akijibu suali la msingi liloulizwa na Mwakilishi wa jimbo la Muyuni Mhe, Jaku
Hashim Ayoub,alipotaka kujua ni kwa nini Serekali haiyoni haja ya kutunga
sheria ya kulinda utamaduni mzuri wa kuheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa
wale wanaovuja sheria kwa makusudi.
Sambamba na hilo
lakini mwakilishi huyo alitaka kujua Serekali inatoa kauli gani unapofika mwezi
mtukufu wa Ramadhani kuhusu vitendo hivyo vinavyokwenda kinyume na utamaduni.
Waziri Mbarouk alisema ni wajibu kwa Waislam kuelimishana
mara kwa mara ili kujua zaidi wajibu wao katika mwezi wa Ramadhani na miezi
mengine.
Serekali ya Mapinduzi Zanzibar tokea enzi zilizopita hadi
leo kila unapowadia mwezi Mtukufu wa Ramadhani imekuwa ikitoa kauli juu ya
Wananchi na Waislam kuheshimu mwezi huo.
Alisema kauli ya kwanza hutolewa na Mhe Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, mwezi wa Shaaban na kauli nyegine
hutolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar
ambapo na Mufti wa Zanzibar na Masheikh nao huelimisha jamii kuhusu
utukufu wa mwezi huo na vipi waislam wanatakiwa kuuheshimu.
Waziri Mbarouk alifahamisha kuwa katika kauli hizo
hulazimika hoteli zote zifungwe wakati wa mchana watu wavae nguo zenye stara,
pia kutokula ovyo mchana wasilewe, wasaidiane na kuoneana huruma na
kuheshimiana na kutokana na maagizo hayo kwa kiwango kikubwa yanatekelezwa .
Aidha aliwataka Waislam kuripoti matukio ya aina hiyo ambyo
yatavunja heshima ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
0 Comments