6/recent/ticker-posts

ziara ya viongozi wa wadi za makunduchi ukiendelea nchini sweden.

Ujumbe wa Wadi ya Makunduchi ukiendelea na ziara yake nchini Sweden wakiwa katika msosi wakati wa mapumziko yao baada ya ziara kutembelea sehemu mbalimbali kupata mafunzo ya Utunzaji wa miji, Ulaji pia ulipamba sikuukuu ya Pamoja. Ndugu Simba anaonekana akitafakari jambo kabla ya kukata keki!
Siku ya nne ya ziara ya kikazi ya ujumbe wa wadi za Makunduchi ilitawaliwa na mazungumzo mazito na muhimu kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya wadi za Makunduchi na Manispaliti ya Kiruna. Ujumbe wa Kiruna uliongozwa na ndugu Ove, wa pili kutoka kushoto na ule wa Makunduchi uliongozwa na ndugu Mohamed Muombwa. Miongoni mwa maombi ya wadi za Makunduchi ni maji pamoja na kuiombea hospitali mpya ya Kajengwa madaktari wa kujitolea
Mji wa Makunduchi unakuwa! Ujumbe wa Makunduchi uliona kunahaja ya kutembelea kikosi cha  Uokozi wa majanga mbali mbali ukiwemo moto. Mfanyakazi wa kituo hiki aliuelezea ujumbe wa Makunduchi kuwa kikosi chake kinatilia mkazo zaidi "KUKINGA MAJANGA" (prevention is better than cure!) Kwahivyo kikosi chao hutoa mafunzo maskulini, kwa wazee, vijana na makundi mbali mbali jinsi ya kujikinga na majanga kama moto, kwa mfano.
Mwalimu HAJI KIONGO akijaribu kuvaa vazi la kujihifadhi na moto ambalo huvaliwa na wazima moto wakati wa mapambano na moto.

Post a Comment

0 Comments