Na Mwandishi Wetu.
Serekali ya Mapinduzi Zanzibar imeeleza kuwa bado wakulimawa
zao la mpungawanaendelea kutumia mbegu yampunga ya Nerika licha ya wakilimahao
kutoa kasoro kwa mbegu hizo na baadhi yao
kutokuzitumia mbegu hizo katika kuzalisha zao la Mpunga Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili Zanzibar , Mhe Mtumwa Kheir Mbarak, katikakikao cha Baraza
la Wawakilishi kinachoendelea nje kidogo ya mji wa Zanzibar huko Chukwani.
Kweli wapobaadhi ya wakulima hivi sasa wameacha kutumia
mbegu ya Nerika na kutowa sababu kuwa mbegu hizo ni ngumu wakati wa kupiga,
jambo linalowafanya baadhi yao kuacha kutumia
mbegu hizo, lakini wapo baadhi yao
wanaendelea kutumia mbegu hizo. Alisema.
Alisema licha ya kuwa
na kasoro hiyo ambayo wakulima wameitoa lakini wengi wao wameipokea vyema na
wanaipenda sana .
Hata hivyo Naibu Waziri huyoamesema kuwa hawawezi
kuwalazimisha wakulima kutumia mbegu hiyo
Kwa upande wa ukosefu wa mabwawa na mabibi shamba, alisema
kuwa hivi sasa Serekali ina upungufu mkubwa wa Wataalam hao hasa katika Kisiwa
cha Pemba ambpo alisema hivi sasa tayari Wizara hiyo imeomba kupatiwa ajira
zaWataalam 40 ili angalau kupunguza tatizo hilo .
Alisema kuwa sababu kubwa inayochagia kuwepo kwa ukosefu wa
Wataalamu hao hasa kwa upande wa Pemba, ni pale Bibi Shamba anapoolewa na Mume
kutoka Unguja huomba uhamisho wa kumfuata mumewe.
0 Comments