Na Mwanajuma Mmanga.
WAKATI mwezi mtukufu wa Ramadhani ukiendelea wakulima wa vijiji vya Donge
Vijibweni na Donge pwani,wamelalamikia tabia ya wizi wa mazao iliyoshamiri, kitendo
kinachowarejesha nyuma wakulima.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wanavijiji hao walisema mazao
kama muhogo, ndizi, viazi, mananasi,miwa
na mapapai na mbegu za mihogo ndiyo yanayoibiwa kwa wingi.
Walisema mara nyingi mazao hayo kuibiwa nyakati za usiku wakati wakulima
tayari wakiwa wameshaondoka.
Walisema kutokuwepo polisi jamii ndiko kulikosababisha ongezeko la wizi
huo.
Naye sheha wa shehia ya Donge vijibweni, Abdalla Abrahman Machano, alikiri
kuwepo kwa matukio hayo na kusema vijana wa mitaani ndio wanaoshiriki wizi huo.
Aliwashauri wakulima kushirikiana ili kuhakikisha wanakabiliwa na wizi huo
pamoja na mifugo inayoharibu mazao yao.
1 Comments
Huu wizi wa mazao umeingia hata kule Pemba na zamani Wazanzibari tulikua na Vibaka lakini sio wengi kama hivi.. Hivi sasa tuna hao tunaowaita Nduguzetu wa kutoka Tanganyika hasa vijana wanajitia kuja Unguja na Pemba lakini wengi wao ni Wizi... Na kama tunavojua BAADHI ya Watanganyika hujiita Waislamu lakini vitendo vyao huwa havina tofauti na asiekua muislamu..
ReplyDeleteSuala hili nikuwakamata hao Masheha KOKO ambao wao ndio wanaoingiza Watu wa CCM kutoka Msumbuji na Tanganyika kila Mkoa.. Hivo wakamateni masheha wenu wao ndio wanajua wageni wote waliowapachika uzanzibari