Na Kauthar
Abdalla
SHIRIKA la Umeme
Zanzibar (ZECO) linaendelea kuchukua hatua za kuimarisha huduma zake ili
kuwapunguzia usumbufu wateja wake.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, Msaidizi Ofisa Uhusiano wa shirika hilo,Haji Juma
Chapa, alisema utaratibu ambao ulikuwepo mwanzo umeshapitwa na wakati na
shirika linafanya kila jitihada kuhakikisha linarekebisha hitilafu zilizopo ili
wananchi wapate huduma bora na kwa wakati.
Akizungumzia
ununuzi wa umeme kupitia simu ya mkononi, alisema huduma hiyo haijaanza
kutumika kwa sababu taratibu bado hazijakamilika kwa sababu mfumo unaotumika
kuuzia umeme umeshapitwa na wakati.
Alisema shirika
limeona ipo haja kwa mara ya kwanza kuanza kutoa huduma kwa kutumia mtandao wa
Zantel kwa sababu wanannchi wengi wa Zanzibar wanatumia huduma za kampuni hiyo
na baadae watafikiria kujiunga na mitandao mengine ya simu.
Aidha
alisema kabla ya huduma hiyo kuanza kutumika kutakuwa na kipindi cha majaribio
ambapo kuna idadi ya watu watatumiwa kuanza kutumia huduma hiyo kabla ya
kuingizwa sokoni.
0 Comments