Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wazanzibari wanaoishi nchi za nje (Diaspora) wakati alipowaalika katika chakula maalum cha mchana, Siku ya Jumamosi Aug 9, 2014 katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Wana Diaspora wa Zanzibar wanaoishi nchi za nje wakipata picha ya pamoja katika chakula maalum cha mchana, Siku ya Jumamosi Aug 9, 2014 katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Mwana Diaspora mkongwe Abdalla Said Ali Managing Director wa Z-TECH Center Ltd - IT Solution akiwa na Abubakar Salum Ahmada Director of Marketing Z-TECH Center Ltd - IT Solution
Pichani: Mwana Diaspora mkongwe Abdalla Said Ali Managing Director wa Z-TECH Center Ltd - IT Solution, akiwa na Abubakar Salum Ahmada Director of Marketing Z-TECH Center Ltd - IT Solution Salum pamoja na Cheif wa Swahilivilla Abou Shatry wakipata picha na viongozi wakuu.
Wazanzibar wanaoishi jimbo la California nchini Marekani wakiwa katika chakula maalum cha mchana, Siku ya Jumamosi Aug 9, 2014 katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa, Uwekezaji na Uchumi Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa alipokuwa akizungumza mbambo mbali mbali kuhusu Zanzibar Diaspora na badala yake kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kutoa hutuba yake kwa Wazanzibari wanaoishi Nchi za nje (Diaspora) aliowaalika chakula cha mchana leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar,
Wazanzibari wanaoishi nchi za nje (Diaspora) wakati alipowaalika katika chakula maalum cha mchana, Siku ya Jumamosi Aug 9, 2014 katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisikiliza kwa makini hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa katika chakula maalum cha mchana, Siku ya Jumamosi Aug 9, 2014 katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Abubakar Salum Ahmada Director of Marketing Z-TECH Center Ltd - IT Solution akipata flash baada ya hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Wanadiaspora kutoka Northampton , Uingereza wakipata picha ya kumbukumbu ndani ya viwanja vya Ikulu
6 Comments
Sijafahamu chochote madhumuni ya hao watu wazanzibari kualikwa Ikulu. Je, wametuzidi au wamepungukiwa na nini kuliko akina sisi tunaoendelea kuishi Zanzibar? Lourence 0777458302
ReplyDeleteHawajawazidi wala hawaja pungukiwa kitu ni kawaida tu nchi nyingi viongozi huwaalika wanachi wao kwani hata na hao viongozi wakienda nchi za nje huwa wanaalikwa pia.
ReplyDeleteSiasa za kinafiki mbwana?
ReplyDeleteje munajua kma hao waalikwa Wazanzibar wanaoishi nje wana akili kuliko hao viongozi wa Serikali ya mapinduzi ya mwaka 1964,
kama nyinyi sio wanafiki basi wapatieni nafasi hao ndugu zetu na wale ambao wapo nje waliokuwa hawakubahatika kuja hapo nchini waingie katika ukumbi wa siasa na mpatieni kila mwenye fani yake na uwezo wake kumlinganisha na waziri mmoja baada ya mmoja ,mbunge na mwakilishi ili waje kukuwekezeeni katika siasa wakujengeeni nchi yenu iliyowashinda tokea mwaka 1964,
sio waje kuwekeza kuuza Tongwa, wawekeni katika uwanja wa siasa na wale wenye shahada za juu kule nje za udaktari muwekeni kuwa waziri wa afya ili muone kwa muda mchache mabaliko ya nchi yenu.
angalieni eti huko Africa eti mtoto mdogo kamaliza skuli amefelishwa hata mtihani wa kiswahili pia ambae iti umeungwa bara baada japo mtihani huu wa kiswahili kutungwa zanzibar na mtoto anapofeli akiwa na umri mchanga kabisa,bsi serikali inashidwa kumuendeleza na ule muda wote alioupoteza inabidi akae barazani au watoto wa kike wasubiri kuharibiwa na sio kuoleza tena kama zamani,
mbona huko Afrika kuna kazi nyingi sana kushinda ulaya, munashindwa kuwarejesha watoto woe waliofeli wa miaka mitano iliyopita katik skuli mbalimbali za kazi za ufundi,ukulima,ujenzi hio pia inataka aje mzungu akusimamieni?
munashindwa kutenga vitengo vya serkali vya kubaini vipaji vya watoto na kazi wanazoweza kuzifanya hapo baadae,
mbona kila mtu Mungu S.A amempa kipaji chake ambacho mwingine hana? kipaji chako wewe ni uongo na unjipatia dhuluma kupitia kudanganya watu yaani "SIASA" kama nitakufanyia hichi na kile ukinipa kura yako, na mwisho wake unashindwa kulekeleza ahadi hio ambayo naam itaulizwa tu si mwisho Qur ani haidanganyi.
kwani kun mafundi wangapi wazee ambao wana ujuzi wa hali ya juu wa shughuli zao hapo nchini ambao umri wao ndio unawaaga,kwanini wasitumiwe ujuzi wao kuwa ndio kama mwalimu wa vitendo kwa wanafunzi hao ambao ndio warithi wa fani hio kwa maendeleo ya taifa letu hapo baadae baada ya hao wazee kuondoka,
je watoto wadogo wadogo kila wanapokuwa munawapitisha,mahospitalini,uwanja wa ndege,bandarini,vilimo mbalimbali,majenzi,uvuvi,na mambo mengine mengi yakiwemo teknologia ili kubaini kila mwanafunzi atakuwa na hamu gani ya baadae cha kukifanya ili aanzwe kuandaliwa kwa maendeleo ya taifa letu la baadae? hilo pia linataka mzungu? mwisho wake tunakuwa hatuna wafanyakazi wenye uwezo na mapenzi tokeo huko chini waliotayarishwa kwa kila sekta na mwisho tunawekana tu mtoto wa shngazi na mjomba hata kama hana elimu,
sasa kama kweli sio wanafiki munataka kuwekeza kwa kuwaalika hao wadau wa nje,basi kwanza wekezeni katika siasa kwani ndio sehemu iliyooza kuliko zote karika nchi, na kama hatukubadilika hapo karika siasa za kinafiki basi hao wanaoitwa pia "MWANZA MUTAMPA KIBALI CHA KUMILIKI BUNDUKI? MWISHO MUTAMFANYIA FITNA MUMFUNGE" huko nyuma likuwa ni mtu mzuri n alijulikana alikuwa na Bunduki kama walivyonavyo viongozi wote labda hivi sasa chupi zimeanza kuwabana ndio wamezifukia sehemu wanakozijua wao,lakini je kwasheria ya nchi, ni nani anaruhusiwa kuuza risasi? je muuza risasi kwanini akauza risasi nyingi kwa mtu mmoja? kama alinunua nje je alizipitisha wapi? nadhani hivi sasa sio waziri tena ni mtu wa kawaida, hivyo angepaswa kusachiwa kama wengine,na je kwanini aliruhusiwa kupita na kiasi hicho? na kama alikuwa na risasi hizo tokea alipokuwa VIP hivyo hakuweza kisachiwa,basi kuna viongozi wengine wana mpaka mapomo ya kutupa kwa mkono kama si bazoka yenyewe au wanapitisha unga huku wakifichiana siri, hizi siasa chafu za kinafiki ndio mpasuko mkumbwa na ndio mjirani zetu wa nchi ya pili hapo Bara yaani Tanzania invyofaidika,siasa za ndani ya nyumba yako na familia yako inakushinda,je utaiweza ya jirani yaani Bara au Tanzania na sasa unaanza kuchomoa balaa jingine la kuvuuka mipaka eti Wazanzibar wanaoishi nje, je Bwana wako Bara keshakupa ruhusa ya kufanya hivyo?
kama hakukubadilika katika hizo siasa chafu basi hakuna diasporas wala ushuzi wa mbaazs.
Ebwana hakuna watu wenye papara kama Wazanzibar,yaani hata wakienda kule ulaya wao wanataka ndani ya mwaka mmoja wawe wamejenga,wanabiashara zao binafsi,yaani paparapara tu,
ReplyDeleteZanzibar ni Taifa kama yalvyokuwa mataifa makubwa yaliyosambaratika kama Turkey,Italy,Greece,Persian yaani Iran,Russia yaani zipozipo tu hii leo kama Zanzibar pia ilikuwa katika ukubwa huo wakati wak kwa ukanda wetu huu wa Afrika mashariki kati na kusini mwa Afrika, hebu angalieni tena ile Film ya SPICE OF ZANZIBAR muone jinsi ufalme uivyokwa ukisafirisha mpaka pembo za ndovu kutoka katika nchi tulizozitawala wakati na kusambaza uislam hadi kufikia South Afrika,Msumbiji pembezoni mote mwa bahari hindi sisi ndio tulitawala,kwa wale waliobahatika kusafiri katika miji yote ya habari ya msumbiji utakuta kuna waislamu wazuri wenye destri zinazofanana na Zanzibar, hata hao jirni zetu upande wa pili Bara Jina la DAR ES SALAAM sio jina la kijerumani wala muingereza hilo ni jina ambalo sisi Wazanzibar tuliwapatia na kuenea duniani kote leo hii kwa umaarufu wa jina hilo,
Dasporas mbwana lengo lake hasa kubwa na makusudia haikuanza leo, huo ni mpang kamambe wa wakuu wa nchi ambao walikaa miaka mingi sana kuunga mpango huu ambao sasa hivi ndio wanaanza kutambulishwa wananchi,
Kama ilivyo Zanzibar ni watu wa kwanza kuweza kubadilisha mfumo ya maendeleo katika ukandaa wetu wa Afrika, Mtindo huu wa diaspora ulitumika kwa mara ya kwanza nchini Oman baada ya mapinduzi ambapo raia wote wa Oman waliokuwa wakiishi nchini Zanzibar waliokuwa na nyadhifa na shahada kubwakubwa wao waliporejea kule Mascut ndio waliokuwa mawaziri wa mwanzo wa kuijenga Oman Mpya ambapo hata kadhi mkuu alikuwa ni hayat Sheikh Saleh ambaye ndie alietafsiri msahafu wa mwazo wa kiislam kwa lugha ya kiswahili,
Sasa waOman walinufaika na ufanisini na utendaji wa Wakaazi wake waliokuwa wakiishi nje yaani Zanzibar ikiwa kama makao makuu ya Oman muda huo hivyo leo hii Oman inajivunia na Diasporas hao waliozaliwa au kukulia Zanzibar hivyo huu ni mpango ambao uliwakuna sana viongozi wetu wa nchi miaka nenda miaka rudi na sasa imefanikiwa kufikia kile ambacho ilikuwa ikikitafuta katika mpango huu wa kiaka mingi,
baada ya kuonekana serikali ya nyerere ingeliendelea kuitesa zanzibar kisiasa viongozi wetu kama kawaida ya wazanzibar kuvumbua mbinu mwanzo hata za biashara kule bara n nchi za Afrika mashariki na kati waliona engo ni kuwaondoa vijana kwa kutumia sababu za siasa ili vijana wakase nje na baadae kuja kurudi nyumbani kushika nchi yao na kuendeshe kwa mtindo wa kileo na hata kuizidi Oman kwani Zanzibar sio jangwa kama Oman na wao wamesoma kutoka kwetu sisi,
Sasa hivi ndio Wazanzibar munatakiwa kuwacha papara zenu za maendeleo ya mwaka mmoja,yaani kuona disporas kama ni kitu kipya miongoni mwenu,
hivi sasa tunawaomba kwa kupitia hiso disporas za nje lengo ni kuwapata Wazanzibar wote na kila mmoja na uwezo wake ili Serikali imtumie kuweza kutubailishia nchi kwa kuendeleza kileo,kuna wasomi wengi ambao ni mawaziri wetu wazuri tu,madaktari na wataalamu wa hali ya juu wazanzibar, hivyo tunakuombeni watoto wetu huko nje tumeni kila mmoja diploma zake katika hivyo vitengo ili serikali iweze kujua ni nani na nani mwnye uwezo wa kuwa waziri au mkuu wa wizara gani ili tuondoe huu ubabaishaji wa viongozi wa nchi yetu.
kwahili tunaipongeza serikali kwa kuwa mpange wake huu wa miaka na dahari unakaribia kukamilia na kuanza kuigeuza na kuirejesha Zanzibar katika heshma yake iliyopotea.
mimi na wewe ndio wajenzi wa Zanzibar mpya.
Ebwana we hakuna watu wenye papara kama Wazanzibari,yaani hata wakienda kule ulaya wao wanataka ndani ya mwaka mmoja wawe wamejenga, wanabiashara zao binafsi,yaani paparapara tu.
ReplyDeleteZanzibar ni Taifa kama yalivyokuwa mataifa makubwa yaliyosambaratika kama Turkey, Italy, Greece,Persia yaani Iran,Russia yaani zipozipo tu hii leo kama Zanzibar pia ilikuwa katika ukubwa huo wakati wak kwa ukanda wetu huu wa Afrika mashariki kati na kusini mwa Afrika.
Hebu angalieni tena ile Film ya SPICE OF ZANZIBAR muone jinsi Zanzibar ilivyoweza kuzitawala nchi nyingi na wakati huo huo kusambaza uislam hadi kufikia South Afrika, Msumbiji pembezoni mote mwa bahari hindi sisi ndio tulitawala.
Kwa wale waliobahatika kusafiri katika miji yote ya habari ya msumbiji utakuta kuna waislamu wazuri wenye desturi zinazofanana na Zanzibar.
Hata hao jirani zetu upande wa pili Bara Jina la DAR ES SALAAM sio jina la kijerumani wala muingereza hilo ni jina ambalo sisi Wazanzibar tuliwapatia na kuenea duniani kote leo hii kwa umaarufu wa jina hilo.
Diaspora lengo lake hasa kubwa na makusudia hayakuanza leo, huo ni mpango kamambe wa wakuu wa nchi ambao walikaa miaka mingi sana kupanga mpango huu ambao sasa hivi ndio wanaanza kutambulishwa wananchi.
Kama ilivyo Zanzibar ni watu wa kwanza kuweza kubadilisha mfumo ya maendeleo katika ukandaa wetu wa Afrika, Mtindo huu wa diaspora ulitumika kwa mara ya kwanza nchini Oman baada ya mapinduzi ambapo raia wote wa Oman waliokuwa wakiishi nchini Zanzibar waliokuwa na nyadhifa na shahada kubwakubwa wao waliporejea kule Muca ndio waliokuwa mawaziri wa mwanzo wa kuijenga Oman Mpya ambapo hata Kadhi Mkuu alikuwa ni hayat Sheikh Saleh ambaye ndie alietafsiri msahafu wa mwazo wa kiislam kwa lugha ya Kiswahili.
Sasa waOman walinufaika na ufanisi na utendaji wa Wakaazi wake waliokuwa wakiishi nje yaani Zanzibar ikiwa kama makao makuu ya Oman muda huo hivyo leo hii Oman inajivunia na Diasporas hao waliozaliwa au kukulia Zanzibar.
Hivyo huu ni mpango ambao uliwakuna sana viongozi wetu wa nchi miaka nenda miaka rudi na sasa imefanikiwa kufikia kile ambacho ilikuwa ikikitafuta katika mpango huu wa miaka mingi,
baada ya kuonekana serikali ya nyerere ingeliendelea kuitesa zanzibar kisiasa viongozi wetu kama kawaida ya wazanzibar kuvumbua mbinu mwanzo hata za biashara kule bara n nchi za Afrika mashariki na kati waliona lengo ni kuwaondoa vijana kwa kutumia sababu za siasa ili vijana wakasome nje na baadae kuja kurudi nyumbani kushika nchi yao na kuendesha kwa mtindo wa kileo na hata kuizidi Oman kwani Zanzibar sio jangwa kama Oman na wao wamesoma kutoka kwetu sisi.
Sasa hivi ndio Wazanzibar munatakiwa kuwacha papara zenu za maendeleo ya mwaka mmoja,yaani kuona diasporas kama ni kitu kipya miongoni mwenu,
Hivi sasa tunawaomba kwa kupitia hizo diasporas za nje lengo ni kuwapata Wazanzibar wote na kila mmoja na uwezo wake ili Serikali imtumie kuweza kutubadilishia nchi kwa kuendeleza kileo.
Kuna wasomi wengi ambao ni mawaziri wetu wazuri tu,madaktari na wataalamu wa hali ya juu wazanzibar, hivyo tunakuombeni watoto wetu huko nje tumeni kila mmoja diploma zake katika hivyo vitengo ili serikali iweze kujua ni nani na nani mwnye uwezo wa kuwa waziri au mkuu wa wizara gani ili tuondoe huu ubabaishaji wa viongozi wa nchi yetu.
Kwahili tunaipongeza serikali kwa kuwa na mpango wake huu wa miaka na dahari unakaribia kukamilia na kuanza kuigeuza na kuirejesha Zanzibar katika heshma yake iliyopotea.
Mimi na wewe ndio wajenzi wa Zanzibar mpya.
Hakuna mtu mwenye papara bwana,hizo ni siasa zako,wazanzibari ni wachapa kazi, Kwani kujenga bei gani? Miezi sita bangalore umemaliza, kwa Samani ya pounds
ReplyDeleteHalafu Ndugu yangu serikali yetu haiangalii usomi au mchango wako kwa ajili ya taifa, kama sio mkereketwa wa ccm mwenye kutii amri ya bwana zetu tanzania hupati lolote, peleka degree zako zote Ikulu.
Pili hao viongozi hujidai tu, Nilikuwa zanzibar mimi na nilitaka kuomba kipande cha ukaazi ilikuwa shughuli kubwa, kisa sio mkaazi wa zanzibar wakati me ni mzanzibar mzaliwa, Sasa jee Mbona muna tuekea vikwazo kupata hivyo vipande? Huwezi kumiliki ardhi bila ya Id ya uzanzibari.