6/recent/ticker-posts

Hitilafu ya Umeme yaunduza Mtambo wa kupokelea mawasiliano wa Zantel Pemba.

Mnara wa kurushia na kupokea mawasiliano ya simu ya kampuni ya Zantel kisiwa ni Pemba umepata hitilafu ya umeme na kusababisha mtambo huo kupata hitilafu ya umeme katika mnara huo ulioko katika moja ya jengo katika mji wa Chakechake jirani na marikiti kuu ya chake hutumiwa na wananchi kupata bidhaa na usafiri wa magari ya abiria katika kituo kikuu cha Chakechake, wakati hitilafu hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa, hitilafu hiyo ya umeme inasemekana na mashuhuda kuwa imetokea muda wa saa tisa mchana.(Picha Abdi Suleiman,Pemba)
 Kikosi cha Zimamoto Pemba wafanikiwa kuuzibiti moto huo na kufanikiwa kuuzima bila ya kuendelea kuleta madhara ya mtambo huo, ulioungua kutokana na hitilafu ya umeme leo mchana
KIKOSI cha Zimamoto na Uokozi (KZU) kisiwani Pemba, kikizima moto uliokuwa ukiwaka katika moja ya mitambo ya Kampuni ya simu za mikononi  Zanteli kisiwani Pemba, uliopo kwenye soko la matunda chake chake Pemba, moto huo haukuripotiwa kuleta maafa kwa wananchi (Picha na Haji Nassor ,Pemba.)

Post a Comment

0 Comments