BIASHARA ya Nguo za Mitumba kama vile shati na
Suruali zimekuwa zikishika kasi katika kuelekea skukuu ya Eid el-fitr, pichani
wananchi wakichagua nguo hizo, katika eneo la wazi mkabala na TRA,ZRB Chake
Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
IKIWA skukuu ya Eid El-Fitr inakaribia wananchi
mbali mbali kisiwani Pemba, wamekuwa wakiwatafutia watoto wao nguo kwa ajili ya
skukuu hiyo, kama walivyokutwa mbele ya soko la matunda Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
ENEO ambalo lilikuwa likitumiwa kwa ajili ya
kuegesha vyombo vya moto maarufu Juwa kali, kwa sasa eneo hilo limekuwa
likitumiwa kwa kufanya biashara za nguo katika kipindi hichi cha kuelekea
Skukuu ya Eid El-Fitr.(Picha na Abdi
Suleiman, PEMBA.)
BIASHARA ya Viatu vya wanaume katika kuelekea skukuu
ya Eid El-Fitr vimepanda bei maradufu, ambapo kwa sasa kiatu kinauzwa kati ya
shilingi Elfu 30,000/= hadi Elfu 28,000/=katika kipindi hiki.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
BIASHARA ya nguo za kiume za watu wazima nazo pia
zimekuwa bei juu, ambapo flana inauzwa kati ya shilingi Elfu 20,000/= hadi Elfu
22,000/= pichani kijana akijisajili kuipokea flana hiyo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)





0 Comments