Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha SUMAIT, Mwinyi Abdalla(katikati) akikabidhi vifaa vya michezo Kepteni wa Timu hiyo Mohammed Suleiman ili kuweza kushiriki vizuri michuano ya Vyuo Vikuu Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Dodoma wiki hii.
Kikosi cha Timu ya Chuo cha SUMAIT Chukwani Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa Vifaa na Uongozi wa Chuo hicho kuweza kushiriki vizuri michuano hiyo.
Na Ali Cheupe.
Kwa upande wake nahodha wa kikosi hicho Mohammed Sleiman ameahidi kuwa wanajua nini ambacho wametumwa na Wana Sumait lakini ubingwa hautokuwa wa chuo pekee bali ni Wazanzibar wote.
Kikosi hicho cha kinachofundishwa na kocha mchezaji wa timu ya waandishi wa habari za michezo Zanzibar (ZASWA) Ali Bakar 'Cheupe' kinaingia kwenye kinyang'anyiro hicho huku wakiwa mabingwa watetezi wa kombe la Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu Zanzibar
Wanandinga walioitwa kupeperusha bendera ya chuo hicho ni: MakipaKassim Zagu na Hamad Shaame.
Walinzi ni: Hamad Yahya, Makame Faki, Mohammed Iddi, Fadhil Khatib, Muhammed Mabrouk na Moh'd Mila.
Viungo ni: Rashid Ramadhan na Moh'd Suleiman, huku washambuliaji akiwa Hamad Rashid na Issa Amour.
Mashindano hayo yanayojulikana kwa jina la TUSA Games yanatarajiwa kuanza Disemba 11 hadi 19 kwa kushirikisha vyuo vikuu Mbali mbali hapa nchini.
0 Comments