6/recent/ticker-posts

MKUTANO WA COP30 WAILTETEA NEEMA TANZANIA, YAPATA MAMILIONI YA DOLA

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Peter Msoffe akifungua Mkutano wa Wadau wa Kupokea Taarifa ya Ushiriki wa Tanzania katika Mkutano COP 30, kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu Wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja Desemba 17, 2025 jijini Dar es Salaam.

Tanzania inatarajia kunufaika na Dola za Marekani milioni 447.12 na Euro 500,000 kutokana na ushiriki wake katika Mkutano wa 30 wa Nchi Wanachama wa Mkataba Mabadiliko ya Tabianchi (COP30) uliofanyika Belem, Brazil hivi karibuni.

Pia, Tanzania itapata kiasi cha Dola milioni 5 hadi 20 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kupitia Mfuko wa Upotevu na Hasara.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Peter Msoffe leo Desemba 17, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Kupokea Taarifa ya Ushiriki wa Tanzania katika Mkutano COP 30, kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu Wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Prof. Msoffe ameeleza kuwa lengo la mkutano huo kuangaza na kujadili fursa mbalimbali katika kuuisaidia jamii katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia miradi ya mazingira inayotekelezwa na Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na wadau.

Aliongeza kuwa Tanzania imeendelea kuimarisha hadhi yake kimataifa kupitia nafasi yake kama Mwenyekiti wa Kundi la Majadiliano la Afrika (AGN) ambapo imewezesha kujadiliwa na kukubalika kwa ajenda ya Nishati Safi ya kupikia, kukubalika kwa hoja ya upatikanaji wa umeme wa bei nafuu kwa watu wote (Mission 300).

“Tumeona hatua nzuri kupitia mkutano huo kama vile Tanzania kufikia maamuzi ya nchi wanachama, kuwezesha Ofisi ya Kanda ya Santiago Network on Loss and Damage ambayo itafunguliwa Dar es Salaam. Tukumbuke hii ni nafasi ya nishati safi ya kupikia kimataifa ni ajenda inayopewa nguvu na uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema.

Kwa upande wa Biashara ya Kaboni, Prof. Msoffe alibainisha kuwa imefanikiwa kupata ufadhili wa misitu ya kitropiki kupitia Mfuko wa Tropical Forest Forever Facility (TFFF).

Ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha usimamizi wa biashara ya kaboni, alitoan wito kwa sekta binafsi kuongeza ushiriki kwenye masoko ya biashara hiyo kwani ina uwezo mkubwa wa ubunifu.

Halikadhalika, aliwaomba wadau hao kuendelea kuandaa miradi ya kimkakati itakayoweza kufadhiliwa chini ya utekelezaji wa Dira 2050 na maamuzi ya COP30, hususan miradi ya uhimilivu, mifumo ya tahadhari mapema, nishati safi ya kupikia na teknolojia, biashara ya kaboni, uhufadhi na usimamizi wa misitu, maji, kilimo na taka.

Kwa upande wake Mshauri wa Rais katika masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira Dkt. Richard Muyungi alisema kuwa miongoni mwa agenda kuu za katika mkutano huo Tanzania iliwasilisha ni pamoja na kupata fedha za mabadikliko ya tabianchi.

Dkt. Muyungi ambaye ni Mwenyekiti wa AGN alisema nchi zilizoendelea zinawajibika kutimiza ahadi zao za kutoa fedha na sio mikopo hizo kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

 Mshauri wa Rais katika masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Majadiliano la Afrika (AGN) Dkt. Richard Muyungi akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa Kupokea Taarifa ya Ushiriki wa Tanzania katika Mkutano COP 30 leo Desemba 17, 2025 jijini Dar es Salaam.


Washiriki wakiwa katika Mkutano wa Wadau wa Kupokea Taarifa ya Ushiriki wa Tanzania katika Mkutano COP 30 leo Desemba 17, 2025 jijini Dar es Salaam.


Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Peter Msoffe (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wakiwa katika Mkutano wa Wadau wa Kupokea Taarifa ya Ushiriki wa Tanzania katika Mkutano COP 30 leo Desemba 17, 2025 jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments