Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Naibu Mwenyekiti wa
Biashara wa Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC) Lord Hugo Swire, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02
Desemba, 2025. Rais Dkt. Samia pamoja na Naibu Mwenyekiti wa CWEIC Lord Hugo Swire ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani Mambo
ya Nje wa ofisi ya Jumuiya ya Madola katika Serikali ya Uingereza walijadiliana
masuala
ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Uwekezaji ambao utachochea ukuaji wa
uchumi na kutengeneza ajira. Aidha, Lord Swire ameomba Tanzania kuwa mshirika wa kimkakati ili kuchochea wawekezaji wengi
kutoka washirika wa Jumuiya hiyo ya Madola. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Mwenyekiti wa Biashara wa Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC) Lord Hugo Swire mara baada ya mazungumzo, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025.


0 Comments