6/recent/ticker-posts

Ujenzi wa Viwanja vya Michezo vya Wilaya na Mikoa ni Muhimu kwa Kuibua na Kukuza Vipaji vya Vijana.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Riziki Pembe Juma, akiambatana na Viongozi wa Wizara hiyo kuangalia utekelezaji wa miradi ya viwanja vya michezo katika Wilaya tofauti  za Unguja.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Riziki Pembe Juma, amesema ujenzi wa viwanja vya michezo vya wilaya na mikoa ni muhimu kwa kuibua na kukuza vipaji vya vijana.

Alisema hayo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya viwanja vya michezo katika wilaya mbalimbali za Unguja ili kuona hatua ya utekelezaji ulipofikia

Waziri ameeleza kuwa ujenzi wa Viwanja hivyo unaendelea vizuri na kuahidi kusimamia  upatikanaji wa vifaa ili kuhakikisha Miradi hiyo inakamilika kwa muda uliopangwa.

Kwa upande wake, Kamishna Idara ya  Michezo Zanzibar Ameir Mohamed Makame amesema kumekuwa na usimamizi nzuri ambao utatoa fursa kwa Vijana kupata nafasi ya kukuza vipaji vyao.

Aidha Kamishna Ameir, ameendelea kuwaomba Wananchi kuitunza miundombinu ya Michezo ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kufikia malengo yaliopangwa na Serikali.

Ziara hiyo imewashirikisha Viongozi mbali mbali wa Wizara ya Habari Sana Utamaduni na Michezo, kwa lengo la  kuona hatua iliyofikia ya utekelezaji  wa Miradi wa Ujenzi wa Viwanja vya Michezo ikiwa ni miongoni mwa viwanja 17 vya  Wilaya na Mikoa ya Unguja na Pemba .


Imetolewa na Kitengo cha Habari .
WHVUM.

Post a Comment

0 Comments