6/recent/ticker-posts

Waziri Mhe. Nadir Amefanya Ziara Kutembelea Ujenzi wa Vituo vya Kupokelea na Kupozea Nishati ya Umeme Zanzibar.

Waziri wa Maji , Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Nadir Abdulllatif  amesema ameridhishwa na ujenzi wa vituo vya kupokelea na kupozea nishati ya umeme hapa zanzibar.

waziri huyo alisema hayo wakati akifanya ziara ya kuangalia ujenzi wa vituo huo unaoendeleo hapa zanzibar .

alisema kuwa ujenzi huo unaendelea kwa kiasi kikubwa umeonesha kukamilika kwa wakati uliyo pangwa kama lengo la serikali linavyoeleza  ili wanachi kupata nishati ya umeme bila ya changamoto yoyote .

Waziri huyo alisema kuwa katika ujenzi huo wa mradi unakuja kuifungua zanzibar katika kupata nishati ya umeme wa uhakika na kuondosha changamoto ya kukatika katika kwa nishati hiyo .

"ujenzi wa vituo hivi ukikamilika kwa kiasi kikubwa upotevu wa umeme hasa kukatika katika utapungua hapa zanzibar " alisema waziri nadir .

alisema kuwa kituo cha welezo kitakuwa kituo kikuu cha kupokea  nishati ya umeme ukitokea fumba na baadae kituo kisambazwa katika kituo cha makunduchi na matemwe ili nishati hiyo kufika kwa wakati bila ya changamoto. 

alisema kuwa serikali ya mapinduzi ya zanzibar imedhamiria kuwa na nishati ya umeme wa hakika ili wananchi kuongeza uzalishaji wa mazao na wafanya biashara na wawekezaji kuongeza idadi ya kuwekeza.

Waziri huyo alisema kuwa wizara hiyo haitomvumilia mkandarasi yoyote anofanya kazi za ujenzi chini ya kiwango na kutoheshimu mkataba wa makubaliano .

"Wizara hii ipo kwa ajili ya wananchi hivyo haiko tayari kumvumilia mkandarasi yoyote atofanya kazi yake chini ya kiwango na kutoheshimu mkataba wa makubaliano " alisema waziri nadir.

Nae naibu waziri wa wizara hiyo Mhe.Seif Kombo Pandu alisema kuwa mradi huo ni moja ya mradi wa kimkakati hivyo kuna kila sababu ya wataalam wa ujenzi kujenga kiwango kinacho ridhisha kwa maendeleo ya watu wa zanzibar .

Alifahamisha kuwa zanzibar hivi sasa shughuli nyingi za uzalishaji zinahitaji zaidi nishati ya umeme hivyo kukamilika kwa mradi huo kutaongeza kasi ya uzalishaji na wananchi kuongeza vipato vyao .

Mapema katibu mkuu wa wizara hiyo Joseph kilangi alisema kuwa mradi ni miongoni mwa miradi  (zesta) ambao ni mkopo kutoka benki ya dunia wenye thamani dola 142 za kimarekani kwa ajili ya miradi hiyo .

Alisema kuwa kuwepo kwa kituo cha kupozea nishati ya umeme na kupokelea  hapa zanzibar kunaenda ondosha upotevu wa nishati hiyo wakati wa kusafiri .

"Vitu hivi ni muhimu sana kujengwa zanzibar kwani umeme katika kusafiri kwake utakuwa haupotei na upatikanaji wake utakuwa mkubwa " alisema kilangi.

Nae mratibu wa mradi wa (zesta) hapa zanzibar maulid shirazi hassan alisema kuwa mradi huo  kwa asilimia 55 ya ujenzi unaenda vizuri hivyo ukikamilika utaenda kuondoa changamoto ya upotevu wa nishati hiyo pamoja na upatikanaji wa uhakika .

Alisema kuwa shirika la umeme kupitia zesta umekuwa na mashirikiano makubwa na wajenzi wa mradi huo ili  kumaliza kwa wakati mradi huo na ubora wake .

Nae mshauri elekezi wa mradi huo suprcevade sahoo kutoka kampuni ya wapcos alisema mradi huo unakwenda vizuri mpaka sasa na asilimia 55 umesha kamilika kwa sasa hivyo aliwatoa hofu viongozi wa wizara hiyo kuwa mradi huo utakamilika kwa wati uliyopangwa .





Post a Comment

0 Comments