Wananchi wa Nanguji na Wazanzibar kwa ujumla wametakiwa kudumisha amani, umoja na mshikamano uliopo nchini ili kuweza kupiga hatua zaidi kimaendeleo.
Hayo yameyasemwa na makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akisalimiana na waumini wa masjid AL-Nassri uliopo Nanguji Mkoa wa kusini Pemba.
Amesema Suala la amani ni suala mtambuka linalomgusa kila mwananchi wa Zanzibar mwenye uchungu na nchi yake hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anaitunza amani iliyopo nchini.
Alhajj Hemed amefahamisha kuwa ili kuendelea kunufaika na maendeleo yaliyopo nchini ni lazima kuhimizana sualala la kuitunza na kuilinda amani iliopo nchini na kuirithisha kwa vizazi vilivyopo na vijavyo ili nao wanufaike na matunda ya uwepo wa amani na utulivu.
Sambamba na hayo, amewataka wananchi kuacha kuhujumiana kwa namna yoyote ile ikiwemo kufanyiana chuki, ubinafsi na vitendo vyenye kuharibu heshima na utu wa mtu wakitambua kuwa wazanzibari wote ni ndugu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewasisitiza wananchi wa Nanguji kuendelea kuelimishana na kuhamasisha juu ya suala zima la umoja na mshikamano ambao ndio nguzo ya kuwepo kwa maendeleo nchini.
Akitoa hutuba ya swala ya Ijumaa Ustadh Ali Mohammed Ali amewataka waumini wa dini ya kiislam kuzidisha mshikamano baina yao hasa katika miezi hii mine bora ukiwemo mwezi huu wa Raajabu ili kuweza kupata fadhila na neema za Mwenyezi Mungu.
Ustadhi ALI amewasisistiza waumini wa dini ya kiislam kuendeleza mshikamano uliopo baina yao pamoja na kuiombea duwa serikali na viongozi wake ili kuweza kutimiza malengo yao ya kuwaletea wazanzibari maendeleo.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Leo tarehe..02.01.2026
.jpg)

0 Comments