Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa awamu ya sita Dkt Amani Abeid Karume amesema Serikali itaendelea kujenga viwanja vya Michezo ili kuweza kuibua vipaji kwa vijana na kuleta maendeleo kwa wanachi wote.
Ameyasema hayo katika ufunguzi wa kiwanja cha Mpira wa Miguu huko Kitogani Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema kujengwa viwanja hivyo ni kielelezo tosha cha kuimarisha na kuibua vipaji vya michezo nchini na kupanua kiwango cha soka kwa vijana.
Aidha amewataka vijana na wananchi kuweza kuyatunza na kuyalinda Mapinduzi ya Zanzibar katika kuyaendeleza kimaadili ili yaendelee kuwa na faida kwa taifa.
Hata hivyo Dkt. Karume amewaasa wananchi wa kijiji hicho kushirikiana kwa pamoja katika kuendeleza na kulinda miundombinu ya Serikali kwa lengo la kuleta maendeleo katika mkoa huo.
Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Ndg. Mattar Zahour ameleza kuwa mradi huo ni muendelezo wa juhudi za Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi katika uimarishaji wa miradi ya viwanja vya Michezo.
Amesema ujenzi wa kiwanja hicho wa mpira ulianza kujengwa kuanzia Septemba 2024 na kukamilika Disemba 2025 ambapo kilijengwa kwa muda wa mizi 16 ambao umejumuisha chumba Cha kubadilishia nguo, Ofisi ya kocha wa mpira, Vyoo, Chumba cha First Aid pamoja na sehemu ya kuweka magari ikiwa uwanja huo una uwezo wa kuchukuwa watazamaji 500 Kwa wakati mmoja. Ambapo kaulimbiu ya mwaka huu
Nae Mkuu wa Mkoa huo Hamida Mussa Khamis amemhukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya utawala wa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuimarisha Mkoa wa Kusini Unguja kuwataka wananachi wa mkoa huo kuwa walinzi wa uwanja huo na kuthamini juhudi za Serikali kwani ndiyo Mkoa pekee uliobahatika kuwa na viwanja vya Michezo vya kisasa kwa ajili ya michezo mbalimbali.
Ameeleza kuwa ufunguzi wa uwanja wa mpira wa miguu Kitogani ni fursa ya kuongeza ajira kwa wananchi wa mkoa huo ni chachu ya maendeleo ya Serikali ili kuendelea kufanya kazi ya kuboresha miundombinu na viwanja vya michezo katika Mkoa wa Unguja na Pemba
Mradi huo wa uwanja wa mpira wa miguu kitogani umegharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 3.2 chini ya kampuni ya Reform Sports ya Uturuki, chini ya Mshauri elekezi AINQ Campan ambao umejumuisha viwanja vya kisasa vya mpira wa miguu na mpira wa mikono, mpira wa kikapu, mpira wa wavu , Tenis, sehemu ya wanariadha ambapo kauli yam waka huu ni "Amani na Umoja ndio dira ya Maendeleo".
.jpg)
.jpg)
.jpg)
0 Comments