Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kujenga Ofisi za Usajili wa Matukio ya kijamii Unguja na Pemba yenye hadhi ili wananchi wapate huduma bora kwa wepesi.
Ameyasema hayo leo huko Mahonda Wilaya ya kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Ofisi za Usajili wa Wilaya ya Kaskazini ‘B’ kufuatia shamrashamra za maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar huduma za Usajili wa makukio ya kijamii zilikuwa zikitokewa katika jengo Moja huko Mambo Msige Forodhami jambo ambalo liliwanyima haki wananchi wa Zanzibar kuzipata haki zao.
“Hati za usajili zilipatikana kwa watu wachache jambo ambalo liliwanyima haki wazawa waliowengi kupata hiki hiyo” ameeleza Waziri Hamza.
Alisema Mapinduzi ya zanzibar yamekuja kuondoa madhila na manyanyaso waliyokuwa wakiyapata wazanzibari na kuwaweka huru kwa kupata haki yao na ndio maana Serikali inajenga vituo vyenye hadhi kila Wilaya ili wananchi wapate huduma bora zenye tija na mafanikio bila ya usumbufu.
"Kabla ya Mapinduzi huduma ya usajili ikipatikana kwa watu maalum tu kusajiliwa nalilikua jengo Moja tu mambomsige ambapo ilikuashida kwa Jamiikupata haki yao"alisema Waziri Hamza.
Waziri Hamza aliwataka wananchi wa Mahonda kuwa tayari kuupokea dhati mradi huo kwani Serikali awamu ya nane ina dhamira ya kuwaletea maendeleo wananchi wake na kuwaondosha usumbufu wa kufuata huduma usajili wa matukio ya kijamii katika maeneo yote nchini.
Aidha Waziri huyo amewataka wakandarasi wa mradi huo kufuata mkataba wa jengo hilo kukamilisha kwa wakati na wenye kiwango.
Akitoa taarifa ya kitaalam Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Malum za SMZ Issa Mahfoudh akitoa ripoti ya kitaalam alisema amesema ujenzi huo ni ahadi ya Dkt. Mwinyi ya kuwasogezea huduma wananchi huduma za kijamii karibu na makaazi.
Amesema kuwa jengo hilo la ghorofa mbili lenye mraba mita 7,732, urefu mita 16 na upana mita 14 ambalo litakua na uzio, sehemu ya kuegesha magari s,sehemu za kusubiria huduma,vyoo sita, nyumba ya mlinzi, Ofisi za wafanyakazi, vyumba vya kumbukumbu, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mwanasheria na kumbi za mIkutano ambalo linajengwa na kampuni ya IPC iliopo Zanzibar na kusimamiwa na ZMA linatarajiwa kumalizika mwezi Agosti 2026 litagharimu zaidi ya shilingi bilioni 1 hadi kukamilika kwake.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja Sururu Juma Sururu amesema Ofisi ya Usajili wa Matukio ya Kijamii ni muhimu sana kwao kwani imewapa matumaini makubwa hivyo kumaliza kwake ni faraja kwao na itarahisisha kuhudumia watu wengi kwa muda mfupi.%20(1).jpeg)
%20(1).jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
%20(1).jpeg)
%20(2).jpeg)
%20(1).jpeg)
0 Comments