Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema imekuwa kawaida kwa baadhi ya Taasisi za kifedha kuftari pamoja na wateja wao na wadau mbali mbali kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina yao.
Ameyasema hayo mara baa ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara ( NBC ) katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinat al Bahri Bweni Zanzibar.
Ameipongeza Benki ya NBC kwa michango ya kifedha, maarifa na ushauri wanaoutoa kwa serikali katika kuhakikisha mipango endelevu ya Serikali inafanikiwa ikiwemo ukuwaji wa uchumi wa Taifa.
Mhe. Hemed amefahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuimarisha mazingira bora na wezeshi ya kufanyia biashara ili kutoa nafasi kwa wawekezaji na Taasisi za kifedha kuja kuekeza sambamba na kufanya kazi zao bila ya usumbufu wa aina yoyote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ahadi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji na wazawa wenye lengo la kushirikiana na Serikali katika kuiletea Zanzibar maendeleo.
Kwa upande wake Bwana Saleh Mohammed Mkuu wa Idara ya Mikopo kutoka Benki ya Taifa ya Biashara( NBC ) amesema Benki ya NBC imekuwa na utamaduni wa kukutana na wateja na wadau wao katika iftari ya pamoja kwa lengo la kudumisha udhirikiano na kujenga ukaribu zaidi wa kibiashara.
Amesema mwezi wa ramadhani unawajenga waumini kuwa na subra, unyenyekevu, uaminifu, kuhurumiana na kutoa kwa ajili ya wasiojiweza ili nao waweze kujikimu katika kipindi chote cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani.
Ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri na wezeshi ya biashara hasa katika sekta za kifedha na kuweka uhuru kwa wawekezaji wandani na nje ya nchi.
Imetolewa na Kitengo cha Habari ( OMPR )
Leo tarehe 27 / 02 / 2026
0 Comments