6/recent/ticker-posts

Waziri wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar Mhe.Nadir Abdullatif Azungumza na Waandishi wa Habari Siku Mia Moja (100) za Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi

Waziri wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar Mhe.Nadir Abdullatif Al-Wardy akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, Siku Mia Moja (100) za Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar leo 4-3-2026. na (kulia kwake) Naibu Waziri wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar Mhe.Seif Kombo Pandu. 


Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Nadir Abdullatif Al-wardy amesema Serikali imeweza kusimamia na kufanikisha miradi ya maendeleo katika sekta zote zilizomo katika Wizara hiyo kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuhusu siku 100 za mafanikio ya uongozi wa awamu ya pili ya Dkt. Mwinyi amesema Wizara hiyo ina sekta muhimu ambazo hugusa moja kwa moja maisha ya wananchi wote.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kuimarisha huduma ya maji katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba ili kuondoa changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama nchini.

“Sekta ya Maji, ni sekta muhimu ambayo hugusa moja kwa moja afya ya jamii, utalii, viwanda, maendeleo ya miji na maisha ya kila siku ya wananchi hivyo kupitia mradi uliofadhiliwa na Benki ya EXIM ya India, takriban kaya 17,726 ziliungwa maji majumbani na kunufaika na huduma ya maji safi na salama” amefahamisha Mhe. Nadir.

Sambamba na hayo ameeleza kuwa kutokana na shughuli za ujenzi wa miundombinu ya barabara inayoendelea nchini, kumekuwa na changamoto ya kuharibika kwa mtandao wa maji katika maeneo mbalimbali hivyo Serikali inaendelea na jitihada za kurejesha huduma ya maji katika maeneo yote yaliyopitiwa na ujenzi huo.

Akielezea kuhusu suala la umeme amesema kuwa Wizara kupitia Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) limefanya jitihada za kuboresha miundombinu ya kusambaza umeme kwa kuongeza njia mpya za usambazaji umeme kwa lengo la kupunguza mzigo kwenye laini zilizopo na kuongeza ufanisi wa usambazaji wa umeme.

Mhe. Nadir amefahamisha kuwa Serikali kupitia Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) imepanga mikakati mbali mbali ya kutatua changamoto ya umeme kwa kuimarisha uzalishaji wa umeme kwa kuongeza vyanzo vya uzalishaji (baseload), kupanua na kuboresha miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme ili kupunguza upotevu ili kuongeza ufanisi.

Aidha Shirika litaendeleza matumizi ya nishati jadidifu na teknolojia za kisasa za uhifadhi na usimamizi wa umeme, kuboresha upatikanaji wa umeme Unguja na Pemba ikijumuisha miundombinu ya nyaya za baharini pamoja na kusimamia fidia na maandalizi ya maeneo kwa utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya sekta ya umeme.

Akizungumzia kuhusu Sekta ya Madini Waziri Nadir amesema Serikali bado inaendelea kudhibiti bei ya mafuta na gesi ili kupunguza gharama kwa wananchi, licha ya kupanda kwa bei ya mafuta mara kwa mara duniani kutokana na kupanda kwa viwango vya fedha za kigeni.

“Gharama za uwendeshaji na matukio ya kimataifa kwa nchi ambazo zinazalisha mafuta, Serikali imeendelea kuhakikisha bei ya mafuta Zanzibar inakua himilivu kwa wananchi wote” amefahamisha.

Aidha amewasisitiza wananchi kulinda miundombinu ya maji na umeme na kushirikiana na Serikali katika kuripoti vitendo vya uharibifu pamoja na uchimbaji haramu kwani vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kuelimisha na kuhamasisha jamii dhidi ya vitendo hivyo.

Naibu Waziri wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar Mhe.Seif Kombo Pandu akizungumza na kutolea ufafanuzi kuhusiana na masuala ya maji, wakati  mkutano na Waandishi wa habari kuhusiana na Siku Mia Moja za Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Jijini Zanzibar na (kushoto kwake) Waziri wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar Mhe.Nadir Abdullatif Al-Wardy. 
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano na Waziri wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar Mhe.Nadir Abdullatif Al-Wardy, akizungumzia Siku Mia Moja za Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, mkutano huo uliyofanyika katika Ukumbi Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar leo 4-3-2026.  
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Salum Ramadhan Abdallah akiongoza mkutano wa Waaandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar, wakati Waziri wa Maji Nishati na Madini Zanzibar akielezeo Siku Mia Moja za Uongozi wa Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Mwinyi, mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar leo 4-3-2026.

             








Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano wa Waziri ya Maji Nishati na Madini Mhe.Nadir Abdullatif Al-wardy, akizungumzia Siku Mia Moja (100) za Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi katika kutekeleza Ilani ya CCM, mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar 4-3-2026.

Post a Comment

0 Comments