6/recent/ticker-posts

DK BILAL ALIPOTEMBELEA GHALA LA JESHI



 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni General Abrahamani Shimbo, akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal Mabaki ya Mabomu yaliyoripuka kwenye Ghala la kuhifadhia silaha katika Kambi ya kutunzia silaha ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania Gongolamboto jijini  Dar es salaam, wakati Makamu wa Rais alipotembelea eneo laKambi hiyo leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitembelea sehemu ya Ghala la kuhifadhia Silaha iliyoathirika kwa milipuko ya Mabomu jana jioni katika kambi ya kutunzia silaha ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania Gongolamboto jijini  Dar es salaam leo. wa pili kulia Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Lt General  Abrahamani Shimbo
Mkuu wa Bohari Kuu ya JWTZ C O 511KJ  Kanali Mwanjire, akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal moja ya sehemu zilizoathirika na milipuko ya Mabomu kwenye Ghala la kuhifadhia Silaha  katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania Gongolamboto jijini Dar es salaam jana jioni, wakati Makamu wa Rais alipotembelea eneo hilo leo.

Picha na Amour Nassor VPO

Post a Comment

0 Comments