Wananchi wa shehia ya Wingwi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar DSk Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza nao katika mkutano maalum wa kuwapa pole,kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,na kusababisha kufiliwa na ndugu zao
Naibu Waziri wa Afya Mhe,Sira Ubwa Mamboya, nae alipata muda wa kuwapa pole wananchi wa Wingwi Pemba,waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya meli ya Mv Spice islander hivi karibuni.
Sheikh Ali Rubea wa Wingwi Pemba,akiomba dua wakati wa mkutano wa kuwapa pole wananchi wa Shehia hiyo waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya meli ya Mv Spice Islander hivi karibuni katika mkondo wa Nungwi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa Wingwi Wilaya ya Micheweni Pemba,waliofiliwa na jamaa zao waliofariki kwa ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,hivi karibuni iliyotokea katika mkondo wa Nungwi.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mama Mwanamwema Shein,akiwapa pole wananchi wa Wingwi Pemba,akiwa katika ziara maalum ya kuwapa pole wananchi waliofiliwa na jamaa zao,katika ajali ya meli ya Mv Spice Islander,iliyozama hivi karibuni katika mkondo wa Nungwi.
Picha na Ramadhan Othman, Pemba
No comments:
Post a Comment