Habari za Punde

MKURUGENZI BANDARI PEMBA AITAKA KAMPUNI YA MWANI SEA WEED KUOPOA MWANI NA GARI LILILOZAMA

Na Nafisa Madai-Maelezo Zanzibar

Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Pemba, Hamad Salim Hamad ameitaka kampuni ya mwani Sea Weed kufanya utaratibu wa kuopowa mwani uliozama usiku wa juzi baada ya gari iliyobeba mwani huo kutumbukia baharini.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko ofisini kwake bandari ya mkoani pemba amesema uwamuzi huo uafuatiwa kumalizika kwa zoezi la uokoaji wa gari hapo jana mchana.


Aidha amesema kampuni hiyo haina budi kutafuta utaratibu wa haraka kuondoa mwani huo baharini kwani sasa umekua ukizuia meli zinapotaka kupaki gatini hapo kushindwa kwa sasa.

Mkurugenzi amesema mwani huo wenye uzito wa tani nane ukiendelea kukaa baharini unaweza kusababisha msongamano mkubwa wa meli kwani sehemu kubwa ya gati imechukukuliwa na mwani huo.

Hata hivyo alisema iwapo kampuni hiyo ya mwani itashidwa kuondoa mwani huo kutokana na kuogopa gharama, shirika litafanya kazi hiyo mara moja ili nafasi hiyo iweze kupisha shughuli za bandari kuendelea kama kawaida na kampuni hiyo italazimika kulipa gharama zote kwa shirika.

Sambamba na hayo Mkurugezni Hamad amewataka madereva kuwa waangalifu pale wanapoingia gatini hapo kwa ajili ya kupakia au kushusha mizigo ili kuepusha ajali kama hiyo.

Kwa upande wake mmiliki wa kampuni ya Sea Weed Roja Mori amesema kampuni yake haina pingamizi ya kuondoa mwani kwani alikiri kuwepo kwa mwani huo kutazuia shughuli za gati hiyo.

Hata hivyo alisema mbali na hasara walioipata kwa kutokea kwa ajali hiyo lakini kampuni inafanya utaratibu wa kuondosha na tayari wameshafanya mazungumzo na wazamiaji kwa ajili ya kuopowa na kutupa bahari kuu kwa vile mwani huo utakua haufai tena

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.