Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amemteua Kanal Mstaafu Miraji Mussa Vuai kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Idara Maalum Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee amesema kuwa uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa uwezo aliopewa Rais chini ya kifungu 34(4) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Zanzibar no.2 ya mwaka 2011.
Uteuzi huo umeanza tarehe 07, Oktoba mwaka 2011.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
12/10/2011.
No comments:
Post a Comment