Habari za Punde

KUTOKA BARAZANI - TUTAANZISHA MTAALA WA UVUVI KUPITIA VYUO VYA AMALI

BARAZA la Wawakilishwi limeambiwa kuwa serikali imedhamiria kutekelea ahadi yake ya kuleta mapinduzi ya uvuvi kwa kuanzisha mtaala wa uvuvi kupitia vyuo vyake vya amali.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Said Ali Mbarouk, alitoa uthibitisho huo barazani jana wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Matemwe, Abdi Mosi Kombo, aliyetaka kujua kama serikali ina mpango wa kujenga vyuo vya uvuvi.


Waziri huyo alisema serikali ina mpango wa kuanzisha mtaala huo kwa kushikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kuvitumia vyuo vya amali ambapo tayari hivi sasa wameanza kufanya mazungumzo ili kujua namna ya kuanzisha mitaala hiyo,

Waziri alisema serikali inalizingatia suala la Mwakilishi wa Micheweni, Thubeit Khamis alietaka kujua mpango wa serikali wa kuweka vyuo vya uvuvi katika maeneo yanayokaliwa na wananchi wengi.

Nae Mwakilishi wa Kojani, Mussa Ali Hassan aliuliza kama serikali ina mpango wa kuwapatia vifaa vya uvuvi kwenye ajimbo ili kuwaendeleza wavuvi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.