Siku ya Jumamosi tukijaaliwa ni siku ya Arafah. Ni moja katika masiku muhimu sana kwa Muislamu. Kwa walio Makkah wakitekeleza ibada ya Hajj, hii ni siku adhimu kwani Mtume, Rehma na Amani juu yake amesema katika Hadithi ' Hajj ni Arafah' . Hivyo akiikosa siku hii amekosa Ibada ya Hajj.
Kwa sisi tusiobahatika kuwepo Makkah tunapaswa kuungana na Mahujjaaj kwa kufunga siku hii. Ni moja katika funga zilizokokotezwa (zilizotiliwa mkazo). Na mwenye kufunga siku hii hufutiwa madhambi yake ya mwaka uliopita.
Hivyo shime tujihimu sisi wenyewe na tuwakumbushe wengine kufunga siku hii.
Pia tunawausia waumini kuihuisha tena Sunnah ya kuchinja siku ya Eid Al Adh haa. Ibada hii imetuwacha mkono wengi na tuna uwezo wa kufanya hivyo.Tujifunze umuhimu wa kuchinja, taratibu na mpangilio wake.
No comments:
Post a Comment