Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Rais wa soko la kimataifa la taasisi inayosimamia miradi ya samaki ya { gri } Bwana Thomas Newland alipomtembelea ofisini kwake iliyopo kwenye mji wa Texas nchini Marekani.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Seneta wa jimbo la Houstan,Texas nchini Marekani Bwana Rodney Ellis wakati alipomtembelea ofisini kwake Houston , Texas
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Dr. Sira Ubwa Mamboya akimkabidhi zawadi za mavazi maalum ya Zanzibar Seneta wa Jimbo la Houston, Texas Bwana Rodney Ellis .
Ujumbe wa Zanzibar unaoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ulipokutana na uongozi wa shirika la biashara la Marekani linaloshughulikia kanda ya Afrika { ustr }.
Picha na Othman Khamis Ame, Texas Marekani
No comments:
Post a Comment