Habari za Punde

MABADILIKO YA JINA LA BLOG

Assalaamu 'Alaykum

Tunapenda kuwajulisha wanajikumbuke wote kwamba jina la blog yenu limebadilika kuanzia leo sasa itakuwa inaitwa Zanzinews.

Tumebadilisha jina la blog ili liende sambamba na malengo yaliyokusudiwa ambayo ni kuwapasha taarifa, habari, matukio, picha na fursa kuweza kujua yanayojiri katika visiwa vyetu pamoja na habari ambazo zinaweza kuwa na maslahi kwa visiwa vyetu.

Hakuna kitu chengine kilichobadilika zaidi ya jina tu la blog na tunawashukuru sana kwa kuweza kututembelea, kusoma habari, kuangalia picha, kutoa  maoni (comments) bila ya kuwasahau wote wanaotutumia habari, picha na matukio. Kutuletea na kututumia habari na picha, kutembelea kwenu na kutoa yenu maoni ndiyo msukumo unaotupeleka kuendelea na kazi hii isiyokuwa ya ajira bali ni kujitolea tu.

Pia tunapenda kuwaomba wanajikumbuke aka wanazanzinews kama mna habari zozote ikiwa mko nchi za nje au nyumbani tutumieni ili tuwaelimishe na kuwahabarisha wengine. Tuandikie/tutumie kupitia barua pepe othmanmaulid@gmail.com 

Jisikie huru kutoa maoni kuunga au hata kupinga mabadiliko haya na maoni yenu yatazingatiwa.

Ahsanteni

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.