Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa katika Viwanja vya Msikti wa Bombay Bazar, wakiaza maandamano ya kusherehekea Mwaka Mpya wa Kiislamu wakiungana na Waislam wengine Duniani.kusherehekea mwaka huo.
Hivi ndivyo ndivyo ilivyokuwa katika maandamano ya Mwaka Mpya wa Kiislam yakipita katika mitaa ya Michezani.
Wanafunzi wa Madrasa wakiwa katika maandamano barabara ya Michezani wakielekea katika viwanja
Mashekh.wakisimama kupokea Maandamano ya Waumini wa dini ya Kiislam wakiingia katika viwanja vya sherehe.
Waumini Dini ya Kiislam wakiigia katika viwanja vya Mnazi Mmoja, kwawa na Farasi na Ngamia.
Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakisherehekea kuingia kwa Mwaka Mpya wa Kiislam wakiingia katika viwanja vya Mnazi Mmoja, kusherehekea mwaka huo na kupata Mawaidha kutoka kwa Mashekhe mbalimbali wa Zanzibar.
Wanafunzi na Madrasa wakipiga Dufu katika kusherehekea Mwaka Mpya wa Kiislam.
Wanafunzi kutoka Madrasa za Potoa wakisherehekea kwa aina yake wakipiga Nai, wakiingia katika viwanja vya sherehe Mnazi Mmoja.
Waumini wa Dini ya Kiislam wakisherehekea kwa aina yake kuingia kwa Mwaka Mpya wa Kiislam wakiungana na Waislam wengine Duniani kuadhimisha, wakiingia katika viwanja vya Mnazi Mmoja, wakipokelea na Kadhi Mkuu wa Zanzibar.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamis Haji Khamis, akipokea maandamano ya Wanafunzi wa Madrasa mbalimbali waliohudhuria katika maandamano ya sherehe za Mwaka Mpya wa Kiislam wakiingia katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamis Haji Khamis, akitowa nasaha zake kwa Waumini wa Dini ya Kiislam katika viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni kusherehekea Mwaka Mpya wa Kiislam.
Katibu wa Ofisi ya Mufti Zanzibar Shekh. Soraga akitowa maelezo na kumkaribisha Mgeni Rasmini katika sherehe hizo za kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kislamu Shekh. Khamis Haji Khamis, kuwahutubia Waumini wa Dini ya Kiislam katika viwanja vya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Shekh Othman Maalim, akitowa mawaidha wakati wa sherehe za kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu katika viwanja vya Mnazi Mmoja, na kutowa kutowa kisa cha Wanyama wawili Ngamia na Farasi walifotumiwa na Waislam kupingania Dini.
Amiri wa ZAFA Abdulrahamani Kizito, akitowa maelezo ya maadhimosho ya maandalizi ya sherehe hizo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
kwa kweli ni tukio la kihistoria na ni mwanzo mzuri ni vigumu kueleza upeo wa furaha yangu juu ya tukio hili. waliofikiria na kuandaa jambo hili MUNGU awalipe kila la kheri.
ReplyDeleteWAMA.
Ni jambo zuri, haya mambo zamani yalikua hayashughulikiwi, na ndio maana hata mwamko bado mdogo hebu angalia mahudhurio....madogo!!
ReplyDeletekwa kweli nimasikitiko makumwa kwa kuona waislam wanavyoanzisha vitu vigeni katika uislam
ReplyDeleteSUBHANA LLAH je huu mwaka ndio kwanza unaanza kwetu sisi zama na na nabii Muhammad(s'alla llahu alaihi wasalam) na utawala wa makhalifa nne haukuwepo na kama ulikuwepo mbona wao hawakufanya na kuwaambrisha waislamu kufanya au sisi tunajua zaid kuliko wao jamani tujiepusheni bidaa katika dini.kama dini haikukamilika wakti wao basi hakuna atakaeza kuikamilisha saiv.
ReplyDeleteAstaghfiruLLaah,
ReplyDeleteHii ni dini ya Kiislamu au dini ya Masufi ? Bila shaka Wangazija ndio wenye mambo ya BIDA'AH.
La Haula Wala Quwata Illa Billah.
Njaa inawasumbua Waunguja.
ReplyDeleteMaulidi, Khitma,taarab na upuuzi wote unafanyika katika kisiwa cha la'ana - UNGUJA.
Mungu Awanusuru ndugu zetu na dada zetu Waumini kisiwani na shari ya watu wa Bidaa. Amin.
Hii ni bidaa ya wazi kabisa makhalifa wetu wanne dio waliokaa no kuanzisha mwaka wa ki islam lakini haya hawakuyaleta na wao ni miongoni mwa waumini bora wa mtumewetu salahu alyhiwasalam, sasa sisi tunachukuwa kutoka wapi?
ReplyDeleteMtume wetu katuusia kushikamana na sunna zake na sunna za makhalifa zake na wao hawakulifanya hili jee nyinyi mmelitowa wapi na linaingia katika sunna gani?
Kama halipo katika sunna basi hukumu yake ni UZUSHI jee mtalibeba hili katika migongo yenu?
Nahao wasiojuwa kitu kama mimi ni kufuata mkumbo basi HATA mimi nahisi hasa kama hii ni bidaa iliyo wazi kabisa
nimeamua kuandika kwa kuwa nimewaona viongozi wa maandalizi wa haya 4 ninduguzangu hassa imenisikitisha sana,mmeingia katika kuwaunga mkono MASHIA KATIKA ITIKADIYAO lakini wamekuzidini kidogo akili, wamekuekeeni mwazoni mwa mwaka na wao wanasheherekea mwezi kumi.
USUFI, USHIA NA USHARIFF: ndio ulio kupelekeeni kuliandaa hili poleni sana SUBHANALLAH!!!POLENI NDUGUZANGU
ASALAM ALEYKUM,
ReplyDeleteNI MASIKITIKO MAKUBWA KUONA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA WATU WANASHEREHEKEA MWAKA MPYA,MUHARAM KAMA WANAVYOSHEREHEKEA ;MARAFIDHA;MASIYA HUKO KARBALA IRAQ,.
LA KUSHANGAZA ,MUFTI WETU NDIO MGENI RASMI ,NIMASIKITIKO NDUGU ZANGU WAISLAM , TUSIPOFANYA JITIHADA ITAKUWA HATARI KWA VIZAZI VYETU
TUMUOMBE ALLAH ATUONGOZE KWENYE HAKI ,NA ATUTOWE KWENYE BATLI,AMIN.
asalamu alykum mimi ni mmisri ninataka kufanya kazi ya kufundisha kiarabu katika zanzibar
ReplyDeletejina langu ni abdelhady shaaban my email hady_hady898@yahoo.com
ReplyDeletenabari >002 01120379028
ahsanteni