SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar na wadau mbali mbali nchini, wameombwa kuisaidia taasisi ya Drug Free Zanzibar inayojihusisha kuwasaidia vijana walioachana na matumizi ya dawa za kulevya.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa Drug Free Zanzibar, Suleiman Mohammed Mauly, amesema Serikali na jamii kwa ujumla hainabudi kuwasaidia vijana ambao wameacha matumizi ya dawa hizo na wana vipaji vya aina mbali mbali.
Alisema hivi sasa taasisi hiyo ambayo ndio inayoshughulikia na nyumba wanazoishi waathirika wa dawa hizo 'Sober House' imeanzisha karakana ambayo itawasaidia vijana walioacha matumizi ya dawa hizo.
Alieleza kuwa Sober House zilizoko katika maeneo mbali mbali ya mji wa Zanzibar kumekuwa na vijana wenye ujuzi wa aina mbali mbali ikiwemo ujenzi, uchoraji, ufundi seremala na aina nyengine lakini wamepoteza sifa hizo baada ya kutumuia dawa hizo kwa muda mrefu.
"Vijana waliaocha matumizi ya dawa za kulevya wapo wengi hivi sasa na hawana kazi ya kufanya hivyo kutokana na kuwa wapo wengi wabunifu hasa wa kazi za mikono tumeamua kuwaanzishia karakana itakayowasaidia kujiendeleza katika fani zao na hata kuanzisha taaluma ya msingi kwa
wale ambao hawajawa na ujuzi wa kazi za mikono,” alisema na huku akisisitiz kwamba hiyo ni kwa manufaa yao.
Alifahamisha kuwa wapo baadhi ya watu wamewaahidi kuwapatia msaada huo wa kupata vifaa ambavyo vitawasaidia vijana hao, lakini ni vyema kama misaada ya aina hiyo itatoka kwenye matawi mengi zaidi ili kazi ziweze kufanikiwa vya kutosha.
"Naomba Serikali yetu pamoja na jamii kwa ujumla itusaidie katika kupata vifaa ambavyo vitaweza kuwasaidia vijana wetu kujiajiri wenyewe na sio kukaa viiweni kurudia matumizi ya dawa hizo,"alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha Mwenyekiti huyo amefahamisha kuwa mbali ya vifaa hivyo kwa vijana wa kiume, lakini pia aliomba kupatiwa msaada wa vyarahani kwa upande wa wanawake.
No comments:
Post a Comment