Habari za Punde

KUMI WAKABIDHIWA VITAMBULISHO POLISI JAMII

Na Mwanajuma Said

WANANCHI kumi waliojiunga na polisi jamii katika shehia ya Kiboje Mwembeshauri Wilaya ya Kati Unguja, wametakiwa kuwa wakweli na waaminifu katika kuteleza kazi zao.

Wito huo umetolewa na Afisa Uperesheni wa Jeshi la Polisi Hamadi Said Masoud, wakati akiwakabidhi wananchi hao vitambulisho maalum vya polisi jamii.


Alisema ni muhimu wananchi hao kutotoa siri katika utekelezaji wa majukumu yao, pia alishauri kutovitumia vitambulisho hivyo katika kufanyia mambo maovu.

"Tunakuombeni kutotoa siri katika kazi zenu za polisi jamii na hivi vitambulisho tulivyokupeni hamtakiwi kuvitumia katika mambo maovu,"alifahamisha.

Nae Mkuu wa Polisi Jamii wa shehia hiyo Inspekta Hassan Korineri Kijogoo, aliwataka wananchi hao kutowa woga na kutovunjika moyo ili kupambana vyema na wahalifu.

Alifahamisha kuwa iwapo watakuwa na woga vitendo hivyo viovu havitaondoka katika shehia hiyo kwani wahalifu watapata njia nzuri za kufanya kazi zao.

Nao wananchi hao mara baada ya kupokea vitambulisho hivyo waliahidi kufanya kazi kwa uaminifu na hawatakuwa na muhali kwa mtu yoyote mwenye vitendo viovu.

Mbali na hayo pia wananchi hao walisema kuwa watashirikiana vyema na jeshi la polisi ili kutekeleza vyema majukumu yao, sambamba na kuomba kupatiwa askari walio waaminifu na wasioweza kutowa siri wakati wa kupanga mikakati yao.

"Tunaahidi kutekeleza vyema kazi zote na kutoa ushirikiano mkubwa na nyie lakini pia tunaomba jeshi la polisi lituptie askari waliowaaminifu na wasitoe siri kwa wahalifu kwani kunaweza
kutuhatarishia maisha yetu,"walieleza.

Waliopatiwa vitambulisho hivyo ni Ame Yussuf, James Sungura, Muhammed Ali, Mabruok Ali, Othman Ame, na Muhammed Masoud, Wengine ni Abeid Mustafa, Vuai Hamadi, Rashid Muru na Juma Siji

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.