Na Mwajuma Juma
TIMU ya soka ya BZL imendeleza ubabe katika ligi ya daraja la pili Taifa baada ya hapo juzi kuifunga New Boko bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Kiwanja cha Ziwani Unguja.
Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu ulichezwa majira ya saa 10:00 za jioni ambapo kufatia ushindi huo BZL inaongoza ligi hiyo kwa kufikisha pointi 22 na kufatiwa na Urafiki yenye pointi 19 na
nafasi ya tatu ikikaliwa na Mashambulizi yenye poiti 18.
Bao hilo la pekee liliwekw akimiyani na mchezaji Hussein Ali katika dakika ya 38 za mchezo huo.
Mbali na mchezo huo pia katika kiwanja cha Mao Dze Tung timu ya African Boys ikafungwa kw aidadi kanma hiyo ya bao na timu ya Super Star balo ambalo lilifungwa na Sid Mohammed katika dakika ya 16.
Uwanjani hapo kulikuwa kufanyike michezo miwili lakini mchezo wa saa 8:00 haukufanyika baada ya timu ya Mwakaje kuja na wachezaji wawili na badala yake timu ya mashambulizi kupata ushindi bila ya kutokea jasho.
Katika uwnaja wa Maungani Shangani ilishinda bao 1-0 dhidi ya Kijanja ambalo lilifungwa na Mohammed Mussa dakika 85 huku Fuoni Kipanga akaifunga Strong fire kwa idada kama hiyo ya bao 1-0.
Ligi hiyo inashirikisha timu 22 ambapo mkia wa ligi hiyo unashikiliwa na Mlandege yenye pointi tatu.
Mbali na michezo ya ligi daraja la pili Taifa lakini pia kulifanyika mchezo wa ligi daraja la pili wilaya ya mjini uliowakutanisha Amaan Freshi na Muungano ambapo Muungano ilifungwa mabao 2-0.
Mabao hayo yote mawili yaliweza kuwekwa kimiyani na mchezaji Makame Juma katika dakika za 44 na 52.
No comments:
Post a Comment