Habari za Punde

UTILIANAJI SAINI MAKUBALIANO BAINA YA VYUO VYA SUZA NA INDIANA CHA MAREKANI KUSHIRIKIANA KATIKA KUKUZA KISWAHILI

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Profesa Idris Ahmad Rai, akitiliana saini ya makubaliano ya kushirikiana katika kutowa mafunzo ya Kiswahili, na Mkurugenzi wa Chuo cha Indiana cha Marekani, Kitivyo cha Swahili FlagshipCenter Dk. Alwiya.S.Omar, utilianaji wa saini hiyo umefanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Suza Majestik Zanzibar.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Profesa Idris Ahmad Rai, na Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Indiana Kitivyo cha Swahili Flagship Center, Dk. Alwiya.S. Omar, wakibadilishana mikataba baada ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiana baina ya vyo hivyo viwili. 
 Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Indiana cha Marekani Kitivyo cha Kiswahili Flagship Center, Dk. Alwiya.S.Omar, akitowa maelezo ya vitabu vya kufundishia Kiswahili karika chuo chao, baada ya kumkabidhi Makamu Mkuu wa SUZA Profesa Idris Ahmad Rai,
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Profesa Idris Ahmad Rai, akitowa maelezo jinsi ya nyanja za ushirikiano baina ya vyo hivyo viwili baada ya kutiliana saini, makubaliano hayo yaliofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho Majestik Zanzibar.  
 Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Indiana Kitivyo cha Kiswahili Flahship Center. Dk Alwiya .S.Omar, akielezea ushirikiano wa pande hizo mbili jinsi ya kutowa elimu ya kujifunza kiswahili kwa wanafunzi wa Indiana na kubadilishana Walimu wa Kiswahili wa vyoo hivyo viwili.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala Dk. Ahmada Hamad Khamis, akitowa shukrani kwa niaba ya Chuo chake katika sherehe za utilianaji wa saini na Chuo cha Indiana cha Marekani katika nyenja za Elimu ya Kiswahili.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.