Habari za Punde

Azimio Yaiangukia ZFA

Na Haji Nassor, Pemba

SIKU chache baada ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) taifa Pemba, kuwafungia wachezaji watatu na Katibu wa timu ya Azimio ya Mbuzini, kutokana na kumfanyia fujo mwamuzi, timu hiyo imeamua kuomba radhi.

Katibu aliyefungiwa wa klabu hiyo Hamad Said, ameliambia Zanzibar Leo kwa njia ya simu kuwa, wameiandikia barua ZFA Taifa Pemba, kuomba radhi ili adhabu hiyo ifutwe au kupunguzwa.

Wachezaji waliokumbwa na adhabu hiyo, ni Salum Hamad, Bakar Mohammed na Mohammed Mossi, ambao wanadaiwa Disemba 17 mwaka jana, baada ya kumalizika pambano lao dhidi ya Mila na kufungwa, walifanya fujo na kutishia kumpiga makonde mwamuzi wa mchezo huo Juma Abdallah, wakidai
aliikandamiza timu yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.